Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni limewafikisha mahakamani watuhumiwa watatu waliotambuliwa kuhudika na tukio la mauaji lililotokea mnamo tarehe 03.04.2013 majira ya 11jioni huko Mbezi Beach katika eneo la kwa Mboma.
Watuhumiwa waliofikishwa mahakamani Kisutu leo tarehe 12.04.2013 ni MT.95735 PTE Noah Moses (25) na MT.99170 PTE Raphael Maisha (29) wote ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania kikosi cha 501 KJ. Watuhumiwa mwingine ni Leverian Anatory (40) ambaye ni askari mhambo mkazi wa Kawe mji Mpya.
Watuhumiwa hao ni kati ya watuhumiwa watano ambao walikuwa wamekamatwa awali na baada ya uchunguzi kufanyika ndipo watuhumiwa watatu waliotambulika na mashaidi.
Aidha mtuhumiwa aliyekutwa na kitambulisho bandia cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akijifanya kuwa ni Ofisa mwenye cheo cha Captain ametambulika kwa jina la Tresphory Magella (52), Mfanyabiashara Mkazi wa Tabata Segerea. Mtuhumiwa huyo alikamatwa tarehe 06.04.2013 majira ya saa tatu usiku huko Mwenge kwa ushirikiano wa askari Polisi na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufuatia taarifa zilizokuwa zimepatiakana kumhusu mtuhumiwa huyo alihusika na utapeli wa aina mbali mbali.
Akionyesha moja ya bastola zilizokamatwana watuhumiwa ambapo zilidhaniwa zimeshatumika katika matukio ya uharifu. Vile vile jeshi la polisi limewakamata zaidi ya wasichana wapatao 50 ambao wajihusisha na biashara ya kuuza miili yao (uchangudoa) ambapo leo walifikishwa mahakama ya jiji. Wasichana hao wanaotuhumiwa ni kati ya miaka 18-43.
Mzee Flavian Elias Mkuwa akishuhudia mbele ya waandishi wa habari jinsi bajaji yake ilivyoibiwa na kupatikana kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na ulinzi shirikishi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela akimkabidhi bajaji aliyokuwa ameibiwa Mzee Flavian Elias Mkuwa baada ya kuibiwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es Salaam na Bw. Said Oden ambaye alikuwa ni dereva. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Bw. Flavian Elias alisema kuwa mtuhumiwa aliiba bajaji hiyo yanye namba za usajili T 118 CEJ tarehe 08.04.2013 majira ya saa 1 usiku kwa ushirikiano wa jeshi la polisi na vijana wa ulinzi shirikishi ambao walifanikiwa kuikamata maeneo ya Kimara.
Magari yaliyofanya uharifu yakiwa limekamatwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments: