Walter akiwaburudisha mashabiki.
WASANII
wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq
Bongo Star Search, Norman, Husna, Menina, Wababa, Geofrey na Walter
jana walionyesha wao ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwapagawisha
mashabiki zaidi ya elfu tatu waliohudhuria katika ukumbi wa Club
Maisha Dodoma.
Show
hiyo kali ilianza majira ya
saa tano usiku, kwa mkali kutoka THT, Ali Nipishe anayetamba na kibao
chake cha ‘MY’, na baadaye kumtambulisha Norman Severino ambaye
kwa mara ya kwanza alizindua wimbo wake wa ‘Si Wewe’.
Steji
ilizidi kuwaka moto pale kijana tokea Dodoma, Godfrey Levis
alipopanda kuimba wimbo wake wa ‘MAYA’ na kufuatiwa na malkia
kutoka THT, Linah, aliyeimba nyimbo zake zote kali.
Mashabiki wakimtuza Walter.
Walter na Ben Paul wakiimba pamoja.
Lakini
alikuwa ni mwanadada, Nsami aliyeonyesha kwamba wanawake waliopo
kwenye tasnia wajipange alipopanda kuimba wimbo wa ‘MUONGO’ na
hatimaye mdada wa taarab, Husna akawamaliza wanadodoma kwa kuimba
wimbo wake wa ‘Nawamimina’, huku akisifiwa na wengi kwa uwezo
wake mkubwa wa kulimiliki jukwaa.
Kama
hiyo haitoshi, mashabiki pia waliburudishwa vya kutosha na mwimbaji
bora wa kiume wa mwaka, Barnaba, ambaye aliiimba nyimbo zake kama
Magubegube na Sorry, ambao unafanya vizuri sana sasa hivi na
kuwafanya mashabiki kupiga kelele kwa kumshangilia.
Norman akiimba.
Nsami Nkwabi na Linah wakiimba kwa pamoja.
Ukumbi
ulizidi kulipuka kwa mayowe baada ya Barnaba kumtambulisha mwanadada
mwingine, Menina, ambaye wimbo wake wa Dream tonight unafanya vizuri
kwenye vyomba vya habari hapa nchini. Menina, ambaye alimsaidia
Barnaba kuitikia wimbo wake wa Wrong Number, alionyesha uwezo mkubwa
katika kumiliki jukwaa.
Hadi
wakati mshindi wa tatu wa shindano la EBSS, Wababa Mtuka anapanda
jukwaani kuimba kibao chake cha ‘My Wife’ watu wa Dodoma walikuwa
bado wakishangilia namna alivoonyesha uwezo katika kuimba.
Shabiki akimpongeza Wababa.
Husna akiwapagawisha mashabiki.
Wa
mwisho kabla ya mshindi wa milioni hamsini kupanda alikuwa ni Ben
Paul, ambaye aliwakonga nyoyo mashabiki wake kwa nyimbo zake kali
kama Pete na Samboira kabla ya kumkaribisha jukwaani Walter.
Mashabiki
hao waliokuwa wakimsubiri kwa hamu, walianza kupiga kelele Walter
Walter, kabla ya kuwatuliza kwa
kuimba wimbo wake mpya wa ‘Siachi’ akifuatiwa wimbo wake mwingine
wa ‘Mamy Love’ ambao aliutoa kama zawadi kwa mashabiki zake wa
Dodoma.
Menyninah akishambulia jukwaa
Barnaba akiwaimbisha mashabiki.
Baadhi ya mashabiki waliohudhuria.
Walter
alipata wakati mgumu jukwaani ambapo mashabiki walimuomba azirudie
nyimbo zake zaidi ya mara tatu hali iliyoonyesha kukubalika kwa hali
ya juu.
Mashabiki
wengi wakizungumza baada ya burudani hiyo walionyesha kuwakubali
vilivyo wasanii wa EBSS, huku wakiwatabiria makubwa.
‘Hakika
vijana wana vipaji na wanajua hasa kutoa burudani, wakipewa sapoti
watafika mbali sana’ alisema Maliki Abdul mkazi wa Dodoma
aliyehudhuria burudani hiyo.
Ziara
hiyo ya washindi wa Epiq BSS inaelekea Dar mwisho wa mwezi huu kabla
ya kuelekea Mtwara.
Toa Maoni Yako:
0 comments: