Meneja wa Tigo Bw. William Mpinga (pichani) akielezea jinsi kampuni ya Tigo ilivyoshinda nafasi ya nane duniani kwenye kutoa huduma kwaDar Es Salaam Tanzania 13th February, 2013. Tigo Tanzania imetajwa kuwa miongoni mwa makampuni bora zaidi duniani yenye mahusiano ya karibu na wateja wake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook. Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika la SocialBokers tarehe 7 February, 2013 ambalo lilifanya utafiti wa makampuni 10 bora zaidi duniani yenye uhusiano wa karibu na wateja kwenye mitandao ya jamii kwenye kipindi cha robo ya mwisho wa mwaka 2012. Tigo Tanzania ndiyo shirika pekee la simu kutoka kanda ya Kati, Mashariki na Kusini mwa bara la Afrika lililofikia viwango hivyo vilivyojumuisha makampuni yote bora duniani.

Mitandao ya kijamii inajitokeza kuwa njia rahisi zaidi kwa wateja mbali mbali kupata taarifa, kuomba misaada na kuelimishwa kuhusu bidhaa mbalimbali, na makampuni yaliyo na uhusiano bora na wateja wao na yenye uwezo mkubwa yamechukua fursa hii kuboresha mahusiano na kuwa karibu na wateja wao. Mitandao hii mikubwa ya kijamii duniani kama vile Facebook, hutoa njia m-badala na iliyo bora kwa mashirika yaliyozidiwa ki-huduma na hivyo kutoa fursa kwa watu wa tamaduni mbali mbali kushirikishana kujadili na kueleweshana.

" Tigo Tanzania imeibuka kuwa namba 8 duniani kote kwenye tafiti hizi kutokana na kujikita vilivyo kwenye kuhakikisha kuwa inatoa huduma bora na za kujitosheleza kwa wateja wake.Tunathamini sana wateja wetu na tunahakikisha kuwa tuko pamoja nao wakati wote kila wanapotuhijati. Maendeleo ya kiteknolojia na dijitali yamewezesha kuwepo kwa mijadala mingi kila wakati kwenye mitandao ya kijamii. Tigo kama Kinara wa uvumbuzi wa bidhaa za mawasiliano inatazama changamoto hii kama fursa ya kujiweka karibu zaidi na wateja na kushirikiana nao kwa ukaribu zaidi. Kila tunachofanya Tigo ni kwa ajili ya wateja wetu, hivyo kutambuliwa huku ki-dunia ni fahari kubwa sana kwetu" alisema Ndg. William Mpinga Manager brand ya Tigo.

Kwa mujibu wa shirika la SocialBoker, utafiti wa mashirika yanayojituma zaidi kijamii kwa kipindi cha mwezi Oktoba na Desemba, 2012, umeonyesha kuwa mashirika huwajibika na kujibu hoja kutoka kwa wateja wao haraka zaidi kwenye kurasa za Facebook. Hoja iliyokuwa inajibiwa kwa wastani wa masaa 21 miezi ya nyuma sasa makampuni yanaweza kujibu kwa kipindi cha masaa 19.5 tu kuelekea mwishoni mwa 2012. Shirika la simu la Tigo Tanzania limepata asilimia 87.30% kwa kujibu hoja ndani ya masaa 28.

"Tigo Tanzania mbali ya kujibu hoja za wateja kwenye mitandao ya kijamii inahakikisha kuwa inafanya hivyo kwa ufanisi zaidi kila wakati. Kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kutambua hilo tumefanikiwa kupata heshima hii kubwa. Tutazidi kuongeza ubunifu ili kuboresha huduma na bidhaa zetu, na tunatambua kwamba, ili kutoa huduma stahili, ushiriki wa wateja wetu ni nyenzo muhimu sana. Tumepata mafanikio makubwa tuliyonayo na kufika hapa tulipo leo kwa kuupa utoaji wa huduma bora kipaumbele, na

kwa heshima hii kubwa, tunaahidi kuwa tutajikita kuhakikisha tunaendelea kutoa ufumbuzi wa mawasiliano uliobora zaidi jambo litakalomfanya kila mteja wetu kutabasamu." alihitimisha Ndg Diego Gutierrez, Managa wa Tigo.

Socialboker ndilo shirika linaloongoza duniani miongoni mwa mashirika yanayofanya tafiti na kutoa takwimu kuhusu mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Google+, LinkedIn na You tube. Kwa njia hii inasaidia makampuni uwezo wa kampeni za kijamii za makampuni yao. Tafiti za hivi karibuni zinajumuisha taarifa za Desemba 2012 za ‘Global Social Media Report’ ambapo utafiti mkubwa ulifanywa ukihusisha idadi ya kurasa za Facebook na watumiaji wake kidunia katika mataifa ya Marekani, Uingereza na Brazili. Mengine ni Azerbaijan, Serbia, Mexico, Poland na El Salvador- kwa kutaja machache.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: