Wanaume kuweni makini sana mnapochagua Wanawake wa kuwapenda, ili wawe wake zenu siku si nyingi, Wanawake wa siku hizi wote wanataka ndoa, Vimeo wanaota ndoa, Virukanjia wanaforce ndoa kwa mimba za ghafla na kupitiliza siku zake, imekuwa shida.

Wanawake wa siku hizi wako radhi wajiunge na Kwaya ili waku-impress wewe Mwanamaombi unayesali kupata mke mwema uingie kingi, na usipotulia magotini kuomba ukaanza kuzuzuka na jeki ya sidiria anazopiga kwenye Tindi lake refu kama mkuki wa Kinjekitile akiwa kwenye mazoezi ya kwaya, na vimini anavyovaa ibadani akiongoza nyimbo utajikuta umeoa mke feki.

Wanawake wa siku hizi hawaoni haya kujibadili tabia temporarily ili uwaone Wife Material, anakupa maji huku anapiga goti unajua umeoa Mnyakyusa Ndaga, Malafyale aliyejitunza kumbe unaopoa guberi mwenye Tabia Pana kama Shuka la Gesti.

Kumbuka, Mke ni Waziri Mkuu Kivuli wa Serikali ya Familia yako, ukioa Waziri mkuu Kilaza Serikali yako itaangushwa na Waasi wachache kwa vita vya siku 2 tu vya Msitu wa Pande... Sali sana, Mke mwema hutoka kwa Bwana, sio kwa Kupoke Facebook wala kwa Kum-follow Twitter.

Imeletwa kwenu na Seth Giovanni, 
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mapenzi. 
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: