Ni
muhimu kula mboga mboga na matunda kila siku na hasa wakati wa mlo.
Unashauriwa kula mboga mboga na matunda ya rangi mbali mbali kwani
rangi zinapokuwa za aina mbali mbali ubora huongezeka.
Unashauriwa
kutumia angalau vipimo vitano vya mboga mboga na matunda kila siku.
Mfano
wa kipimo kimoja ni kama ifuatavyo:
- Karoti zilizokatwa katwa na kupikwa-kiasi cha ujazo wa kikombe kimoja cha chai (25mls)
- Mboga za majani zilizopikwa kama mchicha au matembele kiasi cha ujazo wa kikombe kimoja cha chai(250mls)
- Mboga zisizopikwa (kachumbari/saladi) bakuli moja kubwa ujazo unaoweza kuchukua mlo mtu mmoja;
- Chungwa moja,
- Ndizi mbivu kubwa kiasi-moja;
- Tikiti maji kipande kikubwa kimoja;
- Parachichi moja dogo;
- Mapera mawili;
- Juice glasi moja(250mls)
Mfano:
kwa siku moja
asubuhi
hadi usiku unaweza kula kama ifuatavyo, na isambazwe katika siku
nzima: glass moja juisi, mapera mawili, mchicha uliopikwa kiasi cha
ujazo wa kikombe kimoja cha chai(250mls), matembele yaliyopikwa kiasi
cha ujazo wa kikombe cha chai(250mls) saladi bakuli moja.
Je,
ninaweza kutumia juisi badala ya matunda au mboga mboga?
Juisi
halisi ya matunda inaweza kuwa sehemu ya matunda hata hivyo haiwi
badala ya matunda au mboga mboga. Katika vipimo vitano vya mbogamboga
na matunda unavyotakiwa kutumia kwa siku, juisi inahesabika kama
kipimo kimoja tu hata kama umekunywa nyingi kiasi gani. Ina maana
kuwa ni lazima pia kula matunda na mbogamboga kila siku kwani yana
makapi mlo ambayo hayapatikani kwenye juisi.
Matunda
mengine huliwa na maganda yake ambayo huongeza ubora wake. Kwa maana
hiyo, juisi glasi moja kwa siku inatosha ila ukipenda unaweza kunywa
zaidi.
Usikose kufuatilia masomo haya ya afya hapa hapa kajunason blog, Jumamosi tutajifunza;-
Usikose kufuatilia masomo haya ya afya hapa hapa kajunason blog, Jumamosi tutajifunza;-
Tofauti gani kati ya juisi halisi ya matunda na juisi bandia?
Je
unashauriwa kula mayai mangapi kwa siku?
Je,
kati ya maziwa fresh na mtindi yapi ni bora zaidi?
Toa Maoni Yako:
0 comments: