Kijana ambaye jina lake halikufahamika mara moja (pichani) aliyedaiwa kuwa ni mwizi,  alfajiri ya kuamkia Agosti 4, mwaka huu alishambuliwa kichwani kwa shoka maeneo ya Buguruni, Madenge jijini Dar es Salaam na kufariki dunia muda mfupi baadaye.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, siku ya tukio watu watatu wanaodaiwa kuwa ni wezi  walifika katika eneo la Buguruni Madenge katika saluni moja na kutaka kuiba vitu lakini wakakurupushwa na wengine wakakimbia isipokuwa kijana aliyeuawa.
“Siku hiyo mwenye saluni alilala ndani ya saluni hivyo, walipoanza kuvunja mlango aliamka na kuomba msaada kwa majirani ambapo wengine walikimbia na huyu akakamatwa na kumpata haya,” alisema shuhuda huyo kwa sharti la kutoandikwa jina gazetini.

Uwazi lilipofuatilia tukio hilo katika Kituo cha Polisi Buguruni, afisa mmoja alikiri kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa, mwizi huyo alifikishwa kituoni hapo na kuandikiwa hati ya matibabu (PF3) lakini alifariki dunia  kabla hajafikishwa Hospitali ya Amana.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: