Salaam kwako ndugu yangu.
 
Natumai kuwa u-mzima na unaendelea vema na harakati za mapambano ya maisha.. Nami pia.
Sababu pekee ya wewe kupokea UJUMBE HUU BINAFSI siku hii ya leo ni kwa kuwa umekuwa sehemu ya maisha yangu ndani miezi 12 iliyopita ama zaidi. Hivyo ninaposherehekea siku yangu ya kuzaliwa (Aug 10), napenda kuleta ujumbe huu mfupi wa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa namna ulivyoendelea kuwa mmoja wa wale wanaoyafanya maisha yangu kuwa yalivyo sasa. Iwe ni kwa MANENO, MATENDO ama MAWAZO yako.
Nathamini sana uwepo wako na nakuombea mafanikio katika kila lililo jema utendalo ila maisha yako yawe mfano mwema kwa wengine wengi.

Nikumbushe tu kwamba, katika maisha yetu na katika kila jambo tutendalo, "kuna anayetuona kwa mara ya kwanza na / ama mara ya mwisho" na swali ni kuwa TUNAMUACHA NA TASWIRA GANI KUHUSU SISI NA MAISHA YETU?
Unapendwa, Unakumbukwa na UNAOMBEWA MEMA

ASANTE KWA KUWA ULIVYO
      

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: