Waathirika wa dawa la Kulevya Pemba wakimsikiliza Bi. Rahma Al-Kharoosi, alipokua akitoa msaada wa shilingi milioni 10 za kuwasaidia katika kituo hicho cha Pemba.
Bi. Rahma Al-Kharoosi, akizungumza na Mateja wa Pemba.
 
Na Mwandishi wa Jeshi la Polis- Pemba

CHAKECHAKE PEMBA, JUMATANO 03,2011. Watanzania wakiwemo watumiaji wa dawa za kulevya hapa nchini, wametakiwa kuwafichua na kuwataja bila toga wale wote waliopo kwenye mtandao wa kujihusisha na uingizaji, usambazaji na uuzaji wa dawa kulevya ili wakamatwe.

Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa wito
hao na Balozi wa Polisi Jamii nchini Bi. Rahma Al-Kharoosi aliyefuatana na ujumbe kutoka ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutembelea waathirika wa dawa za kulevya Kisiwani Pemba.

Akizungumza na kundi la vijana hao waliopo chini ya uangalizi maalumu wa kituo cha fifadhi kwa watumiaji wa dawa za kulevya kisiwani humo, Bi. Rahma amesema kuwa wakati sasa umefikawa kuwataja wale wote wanaojihusisha na kusambaza dawa hizo kwa jamii.

Bi Rahama ambaye ametoa shilingi milioni kumi kusaidia huduma kwa waathirika wa dawa hizo wanaopata huduma katika kituo cha kuhifadhia vijana hao Kisiwani Pemba, amesema kuwa kama kila kijana aliyeathirika atamtaja yule aliyepelekea yeye kuathirika ni wazi kuwa Polisi watawafuatilia na kuwakamata na hivyo kupunguza tatizo la ongezeko la madawa hayo hapa nchini.

Bi. Rahma amesema kuwa hakuna haja ya kuendelea na dhana kuwa mtu akimtaja mmoja au kundi la watu waliopo kwenye Mtandao wa watu wanaojihusisha na uagizaji, uingizaji, usambazaji na uuzaji wa dawa hizo atauawa.

Amesema dhana hiyo ni potofu na imekuwa ikiwapa kiburi wafanyabiashara hao pamoja na washirika wake kwani inawafanya waonekane wao wana uwezo mkubwa kulikoni Polisi na Serikali nzima.

Amesema kuwa kwa vile wanaoathirika zaidi na dawa hizo ni vijana na wengi wao wakiwemo watoto kutoka familia masikini ambazo zimekuwa zikitegemea kupata mahitaji muhimu ya kujikimu na sasa wanakosa huduma hizo, hakuna haja ya kuendelea kuwaficha watu hao ambao ni sawa na wauaji.

Bi. Rahma amesema kuendelea kuwafichia siri watu hao kwa kuhofia usalama wa watoa taarifa, ni kuendeleza tatizo la ongezeko la dawa hizo na hivyo kuongeza pia ongezeko la vijana tegemezi katika familia duni.

Balozi huyo wa Polisi Jamii nchini, amempongeza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Maalim Seif Shariff Hamadi, kwa juhudi zake katika kukabiliana na tatizo la mihadarati ikiwemo ya kutoka viwandani na yale ya mashambani.

Bi. Rahma, ametaka Juhudi hizo ziungwe mkono na kila mmoja wetu wakiwemo viongozi wengine wa Serikali na vyama vya siasa ili kwa pamoja tuweze kulikomboa taifa letu katika dimbwi la dawa za kulevya.

Bi. Rahma ametoa shilingi milioni kumi kwa kituo hicho ili kusaidia huduma za uhifadhi ikiwemo vyakula na tiba kwa waathirija wa dawa hizo kituoni hao.

Kwa upande wao Mkuu wa Wilaya ya Chakechake Bi Mwanajuma Magid Abdul, na Mwakilishi wa Makamu wa Kwanza wa raisi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Bw. Juma Bakari Alawa, wamesema kuwa Serikali imeweka mikakati ya kupunguza ongezeko la dawa za kulevya visiwani humo.

Wamesema kwamba kwa kupitia Jeshi la Polisi, mikakati ya kuwabaini, kuwapeleleza na kuwabaini wale wote wanaojihusiosha na biashara haramu ya dawa za kulevya hapa nchini.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba ACP Hassan Nassir na Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini Unguja SSP Mkadam Khamis Mkadam, wamewaomba watu wengine wakiwemo wafanyabiasha kujitokeza kusaidia taasisi zinazowahudumia vijana walioathirika na dawa hizo kwani hilo nalo ni sawa na janga la kitaifa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: