Gabriel Mollel.
Wabunifu wa mavazi nchini Tanzania wametakiwa kuacha dharau, majungu na fitina badala yake wasaidiane ili kuiboresha na kuitangaza vyema tasnia hiyo.

Kauli hiyo ilitolewa na mbunifu wa mavazi, Gabriel Mollel wakati akifanya mahojiano na blog hii jijini Dar es Salaam, ambapo mbunifu huyu alisema kuwa ni vyema wabunifu wakajitoa kuiendeleza tasnia hiyo na kuacha tabia ya majungu na fitina.

"Tatizo sio nani kuingia kwenye tasnia hii kwa mara ya kwanza, ni muhimu wewe mwenyewe kujiuliza umeifanyia nini tasnia hii tokea umeingia, tusiwabeze wabuni wachanga eti kwa sababu tu ya umaarufu ulionao, hatutaweza kufika mahali popote tusipokuwa waangalifu tutazidi kubezana kila siku bila sababu za msingi," alisema Gabriel.

Alisema kuwa wakati umefika sasa kwa wabunifu wote kuacha kushindana kwa midomo bali waonyeshe vitendo ili kuweza kuinusuru tasnia hiyo ya mitindo iweze kusonga mbele zaidi na zaidi.

Mwanadada akiwa katika moja ya vazi alilobuni Gabriell.
"Moja ya tatizo kubwa linalofanya tasnia hii ya mitindo kwa hapa Tanzania ishinde kusonga mbele katika kiwango kinachotakiwa ni wabunifu wenyewe kudharauliana, kila mmoja anaona yupo juu sasa inapelekea kutokuwa na umoja thabiti kwenye kazi zetu," aliongeza Gabriell.

Aliongeza kuwa wabunifu wote wanaweza kuijenga Tanzania yenye nguvu na umoja, "Mpaka sasa hivi hatuna vazi la Kitanzania kama nchi za mangharibi, badala ya kutafakari jinsi kupata mavazi kutambulisha Mtanzania tunaendelea kupeperusha majungu,"



Gabriell Mollel ni mmoja ya wabunifu wa mavazi hapa nchini Tanzania ambaye ananembo yake ya Sairiam na amekuwa akitengeneza mavazi ya asili pamoja na viatu.
Viatu ambavyo anavyotengeneza.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: