UTANGULIZI
Itakumbukwa kwamba mnamo tarehe 22 Juni 2011 Serikali, kupitia kwa Waziri wa Fedha na Uchumi wakati akihitimisha Hotuba ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2011/12, ilitoa maagizo kwa EWURA kuchukua hatua mbalimbali zitakazochangia kupunguza bei za mafuta kwa utaja maeneo mengi kama ifuatavyo (tunanukuu):

(a) Ukokotoaji wa thamani ya shilingi kwa kuioanisha na Dola ya Marekani (yaani Exchange rate);(b) Kuondoa au kupunguza wigo wa asilimia 7.5 ambayo makampuni yaliruhusiwa kuwekwa ili kufidia baadhi ya gharama;

(c) kupitia upya misingi ya ukokotoaji wa viwango vya tozo mbalimbali za taasisi za Umma kwa lengo la kubakia na tozo stahili na kwa viwango stahili bila kuathiri majukumu ya udhibiti ma usimamizi yanayofanywa na Taasisi hizo;

(d) kupunguza tozo za kampuni za mafuta ikiwa ni pamoja na gharama za kibenki (yaani Financing Charges); na

(e) Upotevu wa mafuta yanayosafirishwa kwenye meli na gharama ya ukaguzi (yaani inspection fee).  
(mwisho wa kunukuu).
Aidha, mnamo tarehe 4 Julai 2011, EWURA ilianza mchakato kwa kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari kuhusu mchakato wa kupunguza bei za mafuta. Pia EWURA iliandaa dokezo (discussuon paper) lililokuwa na vipengele mbalimbali ambavyo vitapunguzwa na kusambazwa kwa wadau mbalimbali wakiwemo wauzaji wa mafuta hapa nchini.
Wadau mbalimbali walichangia dokezo hilo na kuwasilisha EWURA kwa maandishi na hatimaye mchakato wa utengenezaji wa Kanuni mpya ambayo imepunguza bei za mafuta ulihitimishwa kwa kuitisha Mkutano wa TAFTISHI uliofanyika Julai 22, 2011 katika Ukumbi wa Karimjee
USHIRIKISHAJI WADAU
Mchakato wa kupata maoni ya wadau (taftishi) ulianza tarehe 04 Julai 2011 na kukamilika tarehe 26 Julai 2011. Kwa kawaida, mchakato huu ungechukua siku 81 lakini kutokana na unyeti wa suala hili, Mamlaka ililazimika kuufupisha hadi  siku 23. Wadau walioshirikishwa katika taftishi hiyo ni pamoja na kampuni za mafuta, Baraza la Watumiaji wa Huduma zinazodhibitiwa na EWURA (Consumer Consultative Council), Baraza la Ushauri la Serikali, Taasisi za Umma kama vile TRA, TBS, WMA, TPDC, TPA, SUMATRA, na TIPER.
MATOKEO BAADA Maoni mbalimbali ya wadau yalipokelewa na kuchambuliwa na timu ya wataalam kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo Wizara ya Nishati na Madini,  Wizara ya Fedha na Uchumi, Shirika la Maendeleo ya Mfuta Tanzania (TPDC), Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na EWURA na katika mfumo mzima wa kufanikisha utayarishaji wa kanuni hii mpya, wadau wote walifahamishwa katika mchakato huu kuwa bei mpya zitatolewa tarehe 1 Agosti 2011.

YA KUTANGAZ BEI MPYA

Baada ya kutangaza bei mpya  zilizoanza Agosti 3, 2011 kampuni zilianza mgomo baridi wa kutouza mafuta kutoka kwenye magahala yake. Hata hivyo mgomo huo haukufahamika sana  kutokana na kutokea wakati kukiwa na siku za mapumziko ya muda mrefu yaani taari 6 hadi tarehe 8 Agosti 2011. 

Baada ya kugundua hilo, Bodi ya Wakurugenzi ya EWURA ilikaa Agosti 9, 2011 na kutoa AGIZO LA KISHERIA (ORDER) kwa kampuni nne ambazo zilionekana ndizo kinara wa mgomo husika. Kampuni hizo ni BP (T) Ltd, Oilcom (T) Ltd, Camel Oit (T) Ltd na Engen Petroleum (T) ltd.

Agizo hilo la kisheria lilizitaka kampuni hizotajwa kutekeleza yafuatayo;
Baada ya agizo kutolewa tarehe 9 Agosti 2011, kesho yake kampuni zote zilianza kuuza mafuta kwenye maghala ambapo siku ya kwanza tarehe 10, Agosti 2011 ziliuzwa lita 8,535,700 kutoka kwenye maghala .

Hata hivyo, pamoja na kuuzwa kwa mafuta kwa wingi, bado BP (T) Ltd alionekana kukahidi amri halali ya EWURA kwa kuzingatia Sheria ya Petroli ya mwaka 2008, kifungu 24 (1) kwa kutouzaa mafuta kwenye vituo vyake vyote.
  
HATUA ZINAZOCHUKULIWA

Baada ya kuchambua kwa undani kuhusu suala hili, Bodi ya Wakurugenzi imekutana leo na kuamua yafuatayo:  

USIMAMIZI WA MAFUTA 

IMESAINIWA
Haruna Masebu
MKURUGENZI MKUU

MAMLAKA YA UDHIBITI WA HUDUMA ZA MAJI NA NISHATI (EWURA)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: