Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi-Chakechake Pemba

Michuano ya Polisi Jamii ya kugombe Kombe la Kamishna Mussa wa Polisi Zanzibar Kanada ya Pemba, imeibua vipaji kwa vija walioshiriki katika michuano hiyo ambapo mmoja ya wachezaji kutoka timu ya Shehia ya Makombeni mkoa wa Kusini Pemba Salehe Omari Othuman(18), ameteuliwa kuichezea timu ya dalaja la kwanza Tabnzania Bara ya Afrika Lyion.

Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa mchezaji huyo amechaguliwa na Balozi wa Polisi jamii nchini Bi. Rahma Al-Kharoosi wakati wa fainali ya michuano hiyo iliyofanyika kwenye uwanja wa Madungu Chakechake Kusini Pemba ambapo timu ya Makombeni iliibuka kuwa mabingwa ya michuano hiyo kwa kuifunga timu ya Shehia ya Kizimkazi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa mabao 2-1.

Akizungumza wakati wa fainali za michuano hiyo iliyozishirikisha timu 22 kutoka mikoa miwili ya Kusini na Kaskazini Pemba, Balozi wa  Polisi Jamii hapa nchini ambaye pia ni mmiliki wa Kampuni ya Mafuta hapa nchini ya RBP Bi. Rahma alisema michuano hiyo imesaidia kubaini vipaji vya vijana kama huyo ambaye yeye peke yake aliifungia timu yake mabao 2 katika michuano hiyo.

Naye Mgeni rasmi katika mashnano hayo ambaye pia ni Mkuu wa Wailaya ya Chakechake Bi. Mwanajuma Magidi Abdallah, pamoja na kumpongeza Bi. Rahma kwa, kujitolea kufadhili michezo mbalimbali ikiwemo ya Jeshi la Polisi, amewaagiza Masheha wote katika wilaya hiyo na wilaya nyingine za mikoa ya Pemba kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi na kuunda timu ili kuunganisha nguvu na kuaminiana miongoni mwa vijana.

Bi Mwanajuma amesema kuwa kama kila shehia itaunda vikundi vya vichezo na wakati huo huo vikatumika katika masuala ya ulinzi na utoaji wa taarifa za kihalifu, ni wazi kabisa kuwa hali ya usalama wa taifa letu utaendelea kudumu.

Awali kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba ACP Hassan Nassir, alisema kuwa kwa upande wa Jeshi la Polisi mashindano hayo yamesaidia kuwasogeza wananchi karibu na Polisi na hivyo kurahisisha upatikanaji wa taarifa za wahalifu.

Kwa upande wake, kijana aliyechaguliwa kujiunga na timu ya Afrika Lyion ya Jijini Dar es Salaam, Salehe Omar Othmani, amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya Bi. Rahama ya kumchagua kuwa miongoni mwa watanzania watakaokuwa wakiichezea timu kubwa kama hiyo.

Amesema kuwa ndoto zake zimetimia na anawaomba vijana wenzake kucheza kwa bidii kwani Jeshi la Polisi limeweza kuwakomboa kupitia michezo.

Katika michuano hiyo, Timu ya Makombani iliichapa bila huruma timu ya Kizimbani kwa mabao 2-1 ambapo hadi mapunziko timu zote zilitoka sala ya bila kufungana.

Timu ya Kizimbani ilikuwa ya kwanza kupachika bao katika dakika ya 12 kipindi cha pili kupitia mchezaji wake Nassoro Hamadi.

Hata hivyo bao hilo lilidumu muda wa dakika sita tu ambapo katika dakika ya 18 mchezaji Selehe Omar Othuma aliwanyanyua washabiki wake kwa kusawazisha bao hilo kwa mkwaju safi na kabla ya dakika tano kukamalizika kwa mchezo huo mchezaji Salehe pia aliongeza bao la pili na hadi kipenga cha mwisho Makombeni 2 na Kizimbani 1.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: