Jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 131 kwa tuhuma za kuhusika na vitendo vya kuvunja maduka na kupora, kuchoma moto magari pamoja na kuvunja vioo magari kadhaa wakati wa vurugu zilizotokea na kuhusisha wanamgambo wa jiji, polisi na wafanyabiashara ndogondogo (WAMACHINGA)wanaopinga kuondolewa kwao katika eneo la makoroboi katikati ya jiji la Mwanza.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro (pichani) alisema kuwa watuhumiwa hao ambao baadhi yao walikamatwa na mali walizopora kwenye maduka wanaendelea kuhojiwa ili kubaini ushiriki wao kwenye tukio hilo na hatimaye kuwafikisha mahakama watakaodhibitika kuhusika kwenye vurugu hizo pamoja na uporaji.

Kwa mujibu wa kamanda Sirro, polisi hawahusiki katika kuwajeruhi kwa risasi majeruhi watatu waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando na kwamba uchunguzi umeanza ili kubaini waliowajeruhi ambapo amedai kuwa huenda majeruhi hao walipigwa risasi na mgambo wa jiji ama wamiliki wa maduka.

Kuhusu madai ya vurugu hizo kuchochewa na baadhi ya wanasiasa kamanda Sirro alisema ni mapema mno kuyathibitisha madai hayo na kwamba uchunguzi bado unaendelea na ikithibitika wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: