Waziri wa Mambo ya Kigeni wan chi ya Iceland, Bwana Össur Skarphéðinsson, amesema baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Palestina Bwana Riyad Al-Maliki, huko Ramallah jana kuwa nchi yake itapiga kura kuunga mkono kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina kwenye Umoja wa Mataifa mwezi Septemba mwaka huu.
Hatua hiyo itachukuliwa tu iwapo mazungumzo ya kutafuta suluhu ya mgogoro wa kuanzishwa nchi mbili yaani Israeli kwa upande mmoja na Palestina kwa upande wa pili yatashindwa.
Pia Bwana Skarphéðinsson alitangaza kuipandisha ofisi ya Palestina kuwa ubalozi kamili.Mawaziri wake walitia sani makubaliano ya kisiasa ambayo yataendelea uhusiano wa kisiasda na kiuchumi baina ya nchi mbili hizi.
Skarphéðinsson alikiri kuwa baada ya kutembelea Gaza na kujionea hali mbaya huko, alisisitiza kuwa iko haja ya kuondoa vizuizi vilivyopo huko Gaza.
Maelfu ya mataifa kushinikiza kuvunjwa vikwazo vya Israeli Zaidi ya raia mia sita wa Ulaya na Marekani, wakiwemo watoto na familia zao, wanatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Ben-Gurion uliopo nchini Israeli leo hii Ijumaa kuitikia wito wa ' vikundi kumi na tano vya Palestina .’
Baada ya kuwasili, watatangaza rasmi kuwa watatembelea ardhi ya Palestina inayokaliwa na Israeli kwa kutambua kuwa jumuia ya kimataifa inatambua mipaka ya Palestina na haki ya kuingia.
Msafara huo utaanza leo 8-16 Julai 2011, kwa kuitikia wito wa vikundi vya Wapalestina kuungana nao.
Toa Maoni Yako:
0 comments: