Mamlaka ya udhibiti wa Nishati na Madini nchini EWURA imefunga kituo cha mafuta cha Panone kilichopo Kibaha mkoani Pwani kwa kosa la kuuza mafuta yalichakachuliwa.

Afisa mkaguzi wa mafuta ya petroli wa EWURA Nathaniel Edward alisema kituo hicho kimefungiwa baada kufanya ukaguzi ukaguzi wa kustukiza na kubaini kuwa mafuta yote ya petroli yaliopo katika kituo hicho yamechakachuliwa.

Nathaniel alisema EWURA imempa mmiliki wa kituo hicho muda wa siku saba kupeleka barua ya kujieleza ni kwa sababu gani wanauza mafuta yaliochakachuliwa.

Hicho ni kituo cha tano mkoani Pwani kufungwa kwa kosa la uuzaji wa mafuta yaliochakachuliwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: