Mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011, Raymond Shaban akiwa katika picha ya pamoja na jaji wa shindani hilo Bagdad pamoja na msanii wa kizazi kipya Nick Mbishi.
Mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011, Raymond Shaban akidhihirisha ushindi wake.
Afisa Masoko wa Bia ya Serengeti, Northen Zone Bw. Mdee Waziri akitangaza mshindi katika shindano la Serengeti Fiesta Freestyle pembeni yake ni Mtangazaji wa Clouds Fm Dj Fetty ililofanyika katika ukumbi wa Pamodz jijini humo.
Crew nzima ya Clouds Media ambayo iliongozwa na Mtangazaji wa Clouds Fm, Dj Fetty akiwemo mzee wa Habari na Matukio wa kwanza kulia ambaye pia alisababisha kukuvurumishia habari katika www.cloudsfm.co wakiwa pamoja na mshindi na afisa masoko wa Bia ya Serengeti Bw. Mdee Waziri wa Northen Zone katika Shindano la Serengeti Fiesta Freestyle ililofanyika katika ukumbi wa Pamodz jijini humo.
Msanii wa Hip Hop, Nick Mbishi akitoa Burudani kwa wakazi wa Mbeya waliojitokeza katika fainali ya shindano la Serengeti Fiesta Freestyle lililofanyika katika ukumbi wa Pamodz jijini humo.
Watangazaji wa Clouds Fm Dj Fetty na Ruben Ndege wakimpa mic jaji wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle.
Mtangazaji wa Clouds Fm Dj Fetty akijaribu kupata maoni kwa wakazi wa Mbeya waliojitokeza katika shindani hilo.
Mtangazaji wa Clouds Fm Ruben Ndege akitoa maelezo.
Washiriki wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle wakionyesha umahili wao.
Umati wa wakati wa Mbeya waliojitokeza katika shindano la Serengeti Fiesta Freestyle.
---
Kijana Raymond Shaban amefanikiwa kumewamwaga wenzake wapatao 50 na kuibuka kuwa mshindi wa shindano la Serengeti Fiesta Freestyle 2011 lililofanyika jijini Mbeya.
Shindano la kumtafuta mkali wa Serengeti Fiesta Freestyle jijini Mbeya lilikuwa ni gumu sana maana baada ya kupata washiriki wapatao 50.
Siku ya pili vijana walijitokeza kwa wingi sana na kweli ulifanyika mchujo wakafaulu 18 ambao walifanikiwa kuingia hakuta ya robo fainali.
Baada ya kuwa wamepatikana hao ulifanyika mchunjo na kubakia 18 ambao kati yao wawili waliingia mitini yani hawakujitokeza tena siku iliyofuta.
Vijana walionekana wenye vipaji sana mpaka kuwaweka majaji katika wakati mgumu.
Jaji wa shindano hilo msanii wa muziki wa Hip Hop, Climax alisema zoezi lilikuwa ni gumu kwa vile vijana wamejipanga na wanaonyesha vipaji vyao.
‘Tunamshukuru Mungu kwa kuweza kutufanikisha kumpata mshindi katika zoezi letu na tumelifanya bila ya upendeleo wowote na tulifuata kanuni na vigezo ikiwemo nidhamu ya msanii awapo jukwaani kutotamka maneno ya matusi,”
Aliongeza kuwa vijana wengi walipokuwa wakifreestyle wamekuwa wakitoa lugha chafu jambo ambalo limekuwa likiwapunguzia maksi.
Aliongeza kuwa mshindi wa Serengeti Fiesta Freestyle 2011 kwa jiji la Mbeya litawakilishwa na Raymond Shaban ambaye aliweza kuwamwanga wenzake wapatao 50.
Raymond Shaban ataweza kukutana na wkali wenzake katika shindano hilo litakalofanyika kitaifa Dar es Salaam na kuwakutanisha washiriki wengine kutoka mikoa ya Arusha, Zanzibar, Dodoma na Mbeya.
Nikiripoti kutoka Mbeya, ni mimi ripota wako Cathbert Angelo Kajuna wa Habari na Matukio.
Toa Maoni Yako:
0 comments: