Wizara kukamilisha muswada wa hatimiliki WIZARA ya Viwanda, Biashara na Masoko, imesema iko katika mchakato wa kukamilisha muswada wa mabadiliko ya sheria ya hatimiliki na hakishiriki ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kwa njia ya simu, Waziri wa wizara hiyo, Cyril Chami,(pichani) alilisititiza kuwa, serikali inatambua kilio cha wasanii juu ya uboreshwaji wa sheria ya hakimiliki na hakishiriki ya mwaka 1999 na kwamba, jitihada zinafanyika kufanikisha marekebisho hayo.
“Wizara inatambua kilio cha wasanii na inajali maslahi, wasanii ni kundi muhimu na tunalipa umuhimu na umakini unaostahili, kazi zao zinahitaji kulindwa na kuheshimiwa na kumekuwa na jitihada kuhakikisha hilo linafanyika,” alisema Chami.
Waziri Chami alibainisha kwamba, kuchelewa kwa mchakato wa kupitisha muswada huo, kunatokana na tofauti zilizopo kati ya makundi mawili ya wasanii, lile la muziki na wa fani nyinginezo, ambazo zitajadiliwa katika kikao baina ya wizara mbili.
Wizara hizo ni ile ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na ile ya Viwanda, Biashara na Masoko.

Toa Maoni Yako:
0 comments: