TAMASHA la aina yake la sanaa na muziki asilia wa Tanzania maarufu kama ‘Mzalendo Halisi 2011’ linatarajiwa kuanza kurindima kuanzia Juni 17-19 kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mratibu wa tamasha hilo, Cassius Mlewa, tukio hilo linalosherehekea sanaa, utamaduni na muziki asilia, kwa mara ya kwanza lilifanyika Mei mwaka jana, ambako washiriki walifarijika na mvuto wa uasilia katika tasnia hiyo ulioonekana kwenye jukwaa.
Mlelwa alisema kivutio kikubwa kilitoka kwa Wazazi Cultural Troupe, maarufu kama ‘Segere’, bendi ya Wahahapa (pichani) na wasanii kama Irene Sanga, Che Mundu, Jhikoman, Mrisho Mpoto na Vitalis Maembe.
Mratibu huyo aliongeza kuwa, mwaka huu kunatarajiwa kuwa na vikundi kutoka mikoa ya Mbeya, Dodoma na Morogoro, sambamba na kikundi cha sanaa na utamaduni kutoka Msumbiji.
Pia aliwataja washiriki watakaorudi mwaka huu kuwa ni pamoja na Black Roots, wakiongozwa na ‘Makombora’, bendi yenye msisimko kwenye jukwaa kutoka Zanzibar na Segere.
“Tamasha hili la pili, litaanza siku ya Ijumaa kama ufunguzi rasmi, ambapo kutakuwa na onyesho la bendi mbili na sherehe ya kutoa Ngao Ya Mzalendo. Ngao hii ni maalum kwa kuenzi kazi za muziki na sanaa kutoka kwa wasanii, bendi au vikundi kutokana na mchango wao katika jamii,” alisema.
Aliongeza kuwa, tamasha la mwaka huu pia litapambwa na wasanii wa sanaa za aina mbalimbali, vyakula vya kuvutia, maonyesho ya vitu vya sanaa kama nguo, michezo na vivutio kwa watoto.
Alifafanua kuwa, Juni 17, ambayo itakuwa ni Ijumaa litaanza saa 12 jioni hadi saa 3 usiku, huku siku inayofuata ni saa 4 asubuhi hadi 4 usiku wakati Juni 19 litaanza saa 4 asubuhi hadi saa 3 usiku, ambako viingilio vitatangazwa hivi karibuni.

Toa Maoni Yako:
0 comments: