BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma Music ‘Mambo Hadharani’, imehamishia rasmi maonyesho yake ya kila Jumapili kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo, uliokuwa ukitumiwa na mahasimu wao, Mlimani Park Orchestral ‘Sikinde Ngoma ya Ukae’.

Akizungumza na Blog ya Habari na Matukio jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bendi hiyo, Said Kibiriti alisema kuwa wameishakubaliana kwa maandishi na wamiliki wa ukumbi huo, Shirika la Uchumi na Maendeleo Dar es Salaam (DDC), kufanya shoo kila Jumapili.

Sikinde ilikuwa ikiutumia ukumbi huo kama ukumbi wake wa nyumbani, ikifanya maonyesho ya kila Jumapili tangu mwaka 1978, baada ya kuwa chini ya umiliki wa DDC na ilibadili jina na kuitwaa DDC Mlimani badala ya Mlimani Park la awali.

Kibiriti, aliwaomba mashabiki wa bendi hiyo kujitokeza kwa wingi katika maonyesho yao kila Jumapili kwenye ukumbi huo wa DDC Kariakoo, kwa kuwa unafikika kwa urahisi hata kwa wale wasio na usafiri binafsi.

“Tunapenda kuwaambia wapenzi wa Msondo Ngoma kuwa kuanzia sasa tumehamia rasmi kwenye ukumbi wa DDC Kariakoo katika maonyesho yetu ya kila Jumapili,” alisema Kibiriti.

Hilo linakuwa pigo la pili la Msondo kuipa Sikinde, kwani hivi karibuni ilimtwaa mwimbaji wa siku nyingi wa Sikinde, Shaaban Dede, ingawa mwanamuziki huyo alianzia Msondo, lakini aliimbia Sikinde kwa muda mrefu, kiasi kwamba sauti yake ilikuwa kama alama ya Sikinde.

Sikiliza nyimbo yao iitwayo 'KAZA MOYO'

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: