Bendi kongwe ya muziki wa dansi, Orchestra Bana Maquiz, Jumapili ya Pasaka inatarajia kutimua vumbi zito la burudani kwenye ukumbi wa Mawenzi Garden, Tabata Mawenzi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Kiongozi wa Bana Maquiz, Tshimanga Kalala Assosa (pichani), alisema kuwa wamejipanga kikamilifu kukonga nyoyo za mashabiki wao wa huko katika onyesho hilo.

Aidha, Assosa alieleza kuwa mashabiki pamoja na wapenzi wao wa huko watakaohudhuria onyesho hilo, watapata fursa ya kufaidi uhondo wa burudani pevu ya vibao vyao vilivyotikisa vilivyo huko nyuma.

“Sina shaka wapenzi pamoja na mashabiki wetu wengi wa Tabata Mawenzi wanafahamu kazi yetu tuwapo jukwaani, hivyo nawaomba wafike kwa wingi ili kupata zawadi nono ya Pasaka tuliyowatayarishia,” alisema Assosa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: