Bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia imejigamba kukonga nyoyo za mashabiki wake wakati wa sikukuu ya Pasaka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, meneja wa bendi hiyo, Kelvin Mkinga, aliwataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuanzia kesho katika ukumbi wa Kijiji cha Makumbusho ambako kiingilio ni sh 10,000.
Alisema kwamba katika onyesho hilo pia watatambulisha wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la ‘Chuki ya Nini’.
Aliongeza kuwa Jumapili watafanya bonanza lao la wastaarabu kama ilivyo ada kwa kiingilio cha sh 5,000 na siku itakayofuata yaani Jumatatu ya Pasaka watalindima kwenye ukumbi wa TCC Chang’ombe kwa kiingilio kama hicho.

Toa Maoni Yako:
0 comments: