Msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini, Sunday Mangu maarufu kama ‘Linex’ amewatoa shaka mashabiki wa aina hiyo ya muziki juu ya uwezo alionao katika kuandika mashairi yatakayomweka juu kwa muda mrefu.
Msanii huyo alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akijibu swali kuwa, haofii kupotea masikioni mwa mashabiki wa muziki huo, kutokana na kutoa nyimbo mfululizo kabla ya nyingine kwisha ladha yake miongoni mwa mashabiki wa Bongo fleva, aina pekee ya muziki iliyojikusanyia wadau wengi
Linex alikiri kuwa, soko la muziki huo kwa sasa linakabiliwa na ushindani mkubwa, lakini yeye kwa upande wake analitambua hilo na kuwa, amejipanga kukabiliana na changamoto hiyo na nyinginezo nyingi, ili kuendelea kuwa juu katika sanaa hiyo.
“Muziki ndio kazi niliyochagua kuifanya maishani mwangu. Natambua kila changamoto zilizopo na nimejipanga kukabiliana nazo. Mimi si miongoni mwa wasanii wanaobahatisha kwenye muziki na ndio maana najaribu kuwathibitishia hilo mashabiki. Nitahakikisha wanaamini juu ya uwezo nilionao,” alisema Linex na kuongeza.
“Kuna wasanii waliwabamba vema mashabiki kwa singo moja kali ya kuuzia albamu, kisha wakapotea, kwangu haitokuwa hivyo. Nimedondosha Mama Halima, na kabla haijapwaya, nimetupia kali nyingine ya ‘Moyo wa Subira’. Lengo ni kuwafanya mashabiki watambue uwezo wangu na waamini juu ya kipaji changu. Niko hivyo na nitaendelea kuwa kama nilivyo,” alisisitiza Linex.
Mwishoni mwa mwaka jana, Linex alitoa wimbo wa ‘Mama Halima’ unaoonekana kubamba hadi sasa katika vituo vya radio na televisheni na katika kile kilichotafsiriwa kama kukurupukia soko la muziki huo, hivi sasa ametoa wimbo wa ‘Moyo wa Subira’ ambao wadau wanashauri asingeutoa mapema, kwani umeupoteza uliotangulia.
Aidha Linex alisema kuwa, kwa sasa albamu yake inakaribia kuingia sokoni, ingawa hajaamua rasmi ibebe nyimbo ngapi, sambamba na hizo mbili alizozitoa za ‘Mama Halima’ na ‘Moyo wa Subira’.
Mkali huyu, anayeimba kwa kutumia nguvu zaidi katika nyimbo zake, amebainisha kuwa, albamu yake itakuwa moto wa kuotea mbali na anaamini itafanya vema sokoni.

Toa Maoni Yako:
0 comments: