TANZANIA inatarajia kupata wawekezaji wengi kutokana na nafasi iliyoipata ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa tisa wa uwekezaji Afrika uliohudhuriwa na wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani.

Mwenyekiti wa wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Balozi Elly Mtango(pichani), alisema jijini Dae es Salaam kuwa mkutano huo ni muhimu na unatarajia kuleta wawekezaji wengi kutokana na kuhudhuriwa na wageni wengi.

“Nchi zote za Afrika Mashariki na Jumuiya ya Madola walikuwa hapa, hivyo mategemeo yetu ni makubwa kwani tumeweza kuitumia fursa hiyo kuelezea maeneo ambayo yanahitaji uwekezaji zaidi, ili tuweze kufikia malengo ya nchi yetu,” alisema Balozi Mtango.

Alisema kupitia mkutano huo Tanzania imejulikana na wawekezaji ambao walitaka kufahamu fursa zilizopo katika uwekezaji, ili waweze kuhamasika kuja kuwekeza.

Alisema TIC kupitia mkutano huu itajipanga vizuri, kwa ajili ya kuishauri serikali namna ya kufanya katika kuvutia wawekezaji zaidi ili waweze kuwekeza kwa ufanisi zaidi katika miradi ambayo tayari ilijadiliwa ikiwemo ya kilimo, madini, utalii na nishati.

Naye Waziri wa Biashara kutoka Kenya, Balozi Chirau Mwakwere, alisema mkutano huo ambao umefanyika Dar es Salaam ni utaratibu wa kibiashara wa pamoja ambapo dunia ya leo inalazimu biashara kufanyika katika nchi zote bila vikwazo.

Alisema utaratibu wa nchi za Afrika Mashariki umefungua soko la watu milioni 130 na mazingira hayo sasa ni kivutio kikubwa kwa wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: