Serikali ya Tanzania inatarajia kutenga kiasi kikubwa cha fedha kwenye bajeti zake zijazo, ili zitumike kwa ajili ya watafiti wa ugonjwa wa malaria nchini.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda, alieleza hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa Jukwaa la watafiti hao ulioandaliwa na Taasisi ya Afya ya Ifakara (IHI), na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Malaria (NIMR) wenye lengo la kujadiliana na kushauriana juu ya udhibiti wa ugonjwa huo nchini.
“Wanasayansi na watafiti wetu wanatumia teknologia ndogo kutafuta mbinu za kupambana na ugonjwa wa malaria licha ya changamoto hizo wanafanikiwa kwa kiasi kikubwa katika azma hiyo,” alisema.
Dk. Mponda alisema kutokana na changamoto mbalimbali, serikali iko tayari kuongeza fedha kwenye bajeti zake, ili zitumike kwa ajili ya watafiti hao na k uongeza kuwa watafiti mbalimbali wakiwemo wa Ifakara na NIMR wamefanya kazi kubwa zilizosaidia nchi kupunguza kwa kiasi kikubwa ugonjwa huo.
Hata hivyo, waziri huyo alikiri kwamba ugonjwa wa maralia umepungua kwa kiasi kikubwa maeneo ya mijini ikilinganishwa na vijijini.
Awali, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Ifakara, Dk. Salim Abdulla, alisema katika tafiti nyingi walizofanya kuna matokeo mazuri yenye kumaliza ugonjwa huo.

Toa Maoni Yako:
0 comments: