----
Rose Muhando pia amethibitisha kushiriki tamasha la pasaka litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, April 24, Rose Muhando pia atazitambulisha nyimbo zake mpya kadhaa ikiwemo ile albamu mpya ya muziki wa Injili ya Haleluya Collections Vol 5 itazinduliwa. Kama vile haitoshi katika tamasha hilo pia kutakuwepo na wanamuziki mbalimbali watakaotumbuiza tamasha hilo kama vile Solomon Mukubwa, Upendo Nkone, Annastazia Mukabwa, Bonny Mwaitege, Christina Shusho na wengine kibao. Kubwa zaidi mgeni rasmi wa tamasha hilo atakuwa ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.
Toa Maoni Yako:
0 comments: