Serikali ya Rais Barack Obama ilifanya kila jitihada kuzuia uchunguzi huru wa Umoja wa Mataifa (UN) kuhusu mashambulizi ya Israel katika Gaza.
Balozi wa Marekani katika UN, Bi Susan Rice ndiye aliyeongoza kampeni hiyo kuzuia uchunguzi wa kina wa UN juu ya “uharamia wa kivita” uliofanywa na majeshi ya Israel mnamo mwaka 2008-2009, kwa mujibu wa nyaraka za kidiplomasia zilizofichuliwa na mtandao wa WikiLeaks.
Katika waraka mmoja Rice alizungumza na katibu mkuu wa UN, Bw Ban Ki-moon tarehe 4 Mei, 2009 na akamsihi kuzuia uchunguzi kuhusu mashambulizi ya Israel dhidi ya majengo ya UN huko Gaza.
Katika waraka mwengine, Rice alitoa angalizo kwa mahakama ya jinai ya kimataifa (ICC) akisema kuwa iwapo ingeendelea kuchunguza “uharamia” wa Israel basi uhusiano wake na Marekani ungeharibika.
Kamati ya uchunguzi ya UN, iliyoongozwa na Jaji Richard Goldstone, imeishutumu Israel kwa kosa la jinai ya kivita, kwa kutumia nguvu kubwa kupita kiasi, kulenga makusudi raia na kuwatumia raia kama ngao.
Mashambulizi hayo ya 2008- 2009 yalisababisha vifo vya Wapalestina zaidi ya 1,400, wengi wao wakiwa wanawake na watoto.
Ripoti hiyo ya Goldstone inaweza kusababisha Israel kufikishwa katika mahama ya ICC huko the Hague kujibu mashtaka ya uharamia wa kivita.

Toa Maoni Yako:
0 comments: