Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa
Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) Bi. Debora Charwe amesema, Serikali
ipo katika mchakato wa kuandaa Mpango wa Muda Mrefu wa Lishe wa Taifa (NN-LTP)
ili kuongeza jitihada za sekta mtambuka katika kuboresha utekelezaji wa lishe
kwa kipindi cha miaka 25 ijayo
Bi. Debora ameyasema hayo leo tarehe
30 Juni, 2026 wakati akifungua Warsha ya mafunzo kuhusu kuandaa mpango wa muda
mrefu wa lishe wa Taifa (National Nutrition Long Term Plan 2026-2050) ambayo
inafanyika jijini Dodoma kwa siku tatu kuanzia Juni 30 hadi Julai 02, 2026
Amesema, mafunzo hayo yanatolewa kwa Wataalam kutoka ngazi ya
Wizara mbalimbali kwa lengo la kuwajengea uwezo kuhusu uandaaji wa mipango ya
muda mrefu wa lishe inayojumuisha sekta mtambuka pamoja na kubadilishana uzoefu
kusaidia katika usanifu, muundo na taratibu za utekelezaji wa Mpango wa muda
mrefu wa Lishe wa Taifa.
Vilevile Bi. Debora amefafanua kuwa, mpango huo unaandaliwa chini
ya usimamaizi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Taasisi ya Chakula na
Lishe Tanzania (TFNC) na wadau wengine wa maendeleo kwa kuzingatia haja ya
kuifanya lishe kuwa moja ya kichocheo na kipimo katika kufikiwa kwa malengo ya
Dira ya Maendeleo ya Tanzania kufikia 2050.
Aidha, warsha hiyo
imehusisha Afisa viungo wa lishe kutoka Wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya
Rais, Mipango na Uwekezaji, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Ofisi ya Waziri
Mkuu TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Mahusiano) pamoja na Wizara
ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Wizara ya Maji na
Wizara ya Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
OFISI YA WAZIRI MKUU NA TAASISI YA CHAKULA NA LISHE TANZANIA
KUSHIRIKIANA KUANDAA MPANGO WA LISHE TAIFA










.jpg)




Toa Maoni Yako:
0 comments: