Na Mwandishi Wetu, Michuzi TvMBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani, Mariam Ibrahim amemshuru Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa , Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kupendekeza jina lake na Kamati Kuu ya chama hicho kulipitisha na hatimaye kushinda kwa kura nyingi.
Ametoa
shukrani hizo kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan
alipokuwa akisalimia viongozi mbalimbali wa Chama hicho wakati wa Semina
ya Uongozi na Maendeleo kwa madiwani wote wanawake wa Mkoa wa Pwani.“Nitumie
nafasi hii kwa dhati ya moyo wangu kumshukuru Mwenyekiti wetu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM)Taifa Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kunipendekeza mimi
na Kamati Kuu kurudisha jina langu na kuja katika Mkoa wa Pwani na
kupigiwa kura nyingi.
“Waheshimiwa
madiwani hatujaonana toka Uchaguzi mkuu ulivyopita hivyo naomba
kuchukua fursa hii kuwashukuru nyote kwa kura zenu za kishindo.Nasema
ahsanteni sana,amesema mbele ya madiwani hao pamoja na viongozi wa Mkoa
huo.
Amesisitiza
ameamua kutoa shukrani hizo kwasababu ndio mara yake ya kwanza
wanakutana ambapo ametumia nafasi hiyo pia kuwaaahidi kuendelea
kushirikiana nao na yupo tayari kwa wakati wowote ambao
atahitahika.“Tutakuwa pamoja katika kila hali.”









Toa Maoni Yako:
0 comments: