Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili katika Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu.
Katika taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Bw. Bakari S. Machumu, viongozi walioteuliwa ni:
(1) Bi. Jenifa Christian Omolo – Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.
Kabla ya uteuzi huu, Bi. Omolo alikuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha.
(2) Dkt. Kedmon Elisha Mapana – Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana.
Kabla ya uteuzi, Dkt. Mapana alikuwa Katibu Mtendaji, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa viongozi hao wataapishwa katika hafla itakayofanyika Ikulu Chamwino, Dodoma mnamo tarehe 21 Novemba 2025, majira ya saa 2:00 asubuhi.
Taarifa hiyo imehitimishwa kwa kusisitiza dhamira ya Serikali kuendeleza mageuzi katika usimamizi wa maendeleo ya vijana kwa kuimarisha uongozi na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya kisera na kimkakati.



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments: