Ni nadra sana kwa mwanasiasa wa kiafrika kuamua kutogombea uchaguzi uliopo mbele yake, wanasiasa wetu wengi wanapenda sana kuongoza or madaraka na hawatoki mpaka walazimishwe.
Uamzi wa Kassim Majaliwa, ambaye sasa bado ni Waziri Mkuu wa Tanzania umewashangaza wengi sana ndani na nje ya nchi.
Hatujazoea kusikia busara kama hii ya kuchukua uamzi wa kutogombea tena nafasi ya ubunge ambayo inaaminika na wengi kuwa ni nafasi ya utajiri au ya kujitajirisha, na ndiyo maana inafuatwa na watu wengi hata wenye taaluma yao ya ualimu, uinjinia na uprofesa wa hiki na kile, sambamba na matumizi makubwa ya fedha za kununua kura.
Kwa nchi za wenzetu ambako uongozi wa kisiasa wanauchukulia kama ni utumishi wa umma, suala la uongozi kwao si la kufa na kupona. Watu wengi huko wanaingia kwenye nafasi za kisiasa mara nyingi kwa kufuatwa na wananchi, na wakishakubali watakuja kutekeleza majukumu waliyopewa na wananchi basi, na wakishamaliza tu muda wao hawahangaiki kujiandaa na uchaguzi ujao, wanaacha na kwenda kufanya mambo yao binafsi.
Majaliwa ni nani na yukoje? Sina historia yake ya tangu kuzaliwa na malezi yake ya familia, shule, jamii alimolelewa, zaidi tu nafahamu kuwa yeye ni Mwalimu na ameingia kwenye siasa wakati wa utawala wa Rais Jakaya Kikwete na kuteuliwa kuwa Waziri wa Tamisemi akitokea ualimu, kisha Waziri Mkuu wakati wa Rais John Magufuli kwa vipindi vyote vya awamu ya tano (2015 - 2025).
Kwenye uongozi wake, Majaliwa ameonyesha mambo mengi ya kiuongozi ambayo yamepelekea watanzania wengi kuwa na imano na matumaini naye, kwamba ikitokea akagombea nafasi ya u_rais basi anafaa kuwa Rais wa Tanzania.
Anazo sifa nyingi lakini nitaje chache,
Kwanza, Kassim Majaliwa ni mtu makini na mtulivu na anayependa kuongoza kisayansi na si kisiasa zetu za "michakato, au umbea, majungu, uongo na fitina pamoja na kuviziana".
Pili, Majaliwa ni mvumilivu sana na ni muungwana asiye na papara. Yapo mambo ambayo hata watanzania wameona akifanyiwa lakini kwake hayakuwa kitu, alionesha haiba mpaka hata sasa.
Na kuna wakati aliweza kukemewa na hata kupewa maagizo na watu alioshiriki kuwateua mwenyewe kwenye nafasi walizonazo na akakaa kimya au kufuata hayo maagizo bila ya chuki.
Ni Kassim Majaliwa ambaye, wakati mwingine alikuwa akifanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na wasaidizi wake (mawaziri) lakini alifanya yeye bila kujali udogo wa shughuli yenyewe.
Sitaki kusema mengi, lakini lipo jambo la kujifunza kwa Majaliwa nalo ni kwamba, hakuna kitu kizuri kama kuyaacha madaraka wakati bado yanakuhitaji, na vile vile kuyaachia madaraka ikiwa wananchi bado wanakupenda.
Mungu aendelee kumtunza Kassm Majaliwa wa watanzania, hakika bado tunamhitaji sana ktk taifa letu, kama sio leo basi
Kwiyeya Singu. 0784977072


.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments: