Mwl. Bryceson Makena ambaye ni muasisi wa Kisima amefafanua kuwa kongamano hilo la siku tatu litakuwa na zaidi ya washiriki 1000.
Na Vero Ignatus, Arusha.
Chama cha wafawidhi wa matukio nchini Tanzania (KISIMA CHA MAFANIKIO ) wameandaa kongamano la kuongeza uelewa na maarifa juu ya tasnia nzima ya Washereheshaji itakayoanyika Jijini Arusha kuanzia Aprili 12-14 katika kituo cha Kimaraifa cha Mikutano (AICC) ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Mb) Mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa.
Mwl. Bryceson Makena ni muasisi wa Kisima amefafanua kuwa kongamano hilo la siku tatu litakuwa na zaidi ya washiriki 1000 ,ambapo lengo kuu likiwa ni kutoa mafunzo maalum ya tasnia ya Washereheshaji,ili kujenga ueledi ,katika shughuli za kiserikali ,sekta binafsi ,kijamii pamoja na shughuli za kisiasa na uratibu wa matukio yenye tija kwa taifa.
Mwl. Makena amesema kwa kutambua juhudi za serikali chini ya Rais wa Tanzania Dkt Samia, kuhusiana na tatizo la ajira kwa vijana, kumomonyoko wa maadili na janga la kukosa uzalendo,amesema wao kama wadau wa tasnia husika wameamua kuunga juhudi hizo kwa vitendo kwa kuelimisha, kuhamasisha, kuburudisha, kushauri pamoja na kujifunza sera, miongozo, maelekezo, mipango mikakati na vipaumbele vya kitaifa kupitia majukwaa tunayowasiliana moja kwa moja na jamii kubwa ya watanzania kwenye shughuli na matukio wanayoratibu.
Washiriki mafunzo ya BOT ya namna bora ya kutunza noti na sarafu na uwekezaji katika dhamana za serikali kwa Baraza la Maridhiano la Mkoa wa Dodoma pamoja Washereheshaji kutoka Kisima cha Mafanikio (KCM) Kanda ya Kati katika ofisi za Makao Makuu ya Benki Kuu jijini Dodoma. (Picha kutoka Maktaba).
---
“Chama chetu kina zaidi ya wanachama 450 waliogawanyika kanda 6,na bado tunaendelea kupokea wanachama wapya,mfawidhi wa matukio mmoja anaweza kukutana na watu zaidi ya 1000 kwa wiki katika matukio mawili tofauti ya muda wa kazi na baada ya kazi kwa mwezi anakutana nawatu 4000, fani hii inahitaji mafunzo rasmi na vyeti vya kitaalam tofauti na kauli zilizozoeleka mtaani kwamba vijana wengi wanaingia kwenye fani kwasababu ni kazi rahisi sana ati mdomo haulipi VATna hakuna gharama kubwa ya kuendesha kazi hii zaidi ya kuwa na suti tatu nne,kitu ambacho kinashusha hadhi ya,heshima na thamani ya taaluma’’, alisema Makena.
Hivyo Makena ameiomba serikali kupitia ofisi ya Waziri mkuu kuangalia namna ya kushirikiana nao katika maeneo yafuatayo;Srikali itengeneze mfumo rasmi wa mafunzo ili kuleta tija na weledi katika tasnia,serikali itumie wafawidhi matukio waliorasimishwa rasmi kisheria,kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Vilevile BASATA wawashirikishe TAMISEMI kupitia viongozi wa serikali za mitaa katika kusimamia katika kusimamia maadili ya tasnia kwa kupeleka muongozo sharia na kanuni za uendeshaji wa shughuli hizo.
Ester Kimweri ni mwenyekiti wa Kisima cha Mafanikio amesema hadi sasa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 75 amesema wameamua kufanya kongamano hilo Arusha ili wapate pia wasaa wa kwenda kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi za taifa.
‘’Sisi ni Washereheshaji tutakapofika hifadhini kwanza kunachangia pato la Taifa ,pia tunayofursa ya kutangaza vivutio mbalimbali vilivyopo katiika hifadhi zetu kwa kupitia kurasa zetu mbalimbali za kijamii,vilevile pale tunapopata wasaa tukiwa kwenye utendaji kazi wetu wa kila siku’’alisema Esta.
KCM walishiriki Mafunzo yaliiyofanyika kwa muda wa siku mbili mfululizo (28 na 29 Mei 2024). Siku ya kwanza ilikuwa ni kwa Baraza la Maridhiano la Mkoa wa Dodoma ambalo linaundwa na viongozi wa dini na siku ya pili kwa Washereheshaji. (Picha kutoka Maktaba).
---
Akizungumza mmoja wa wanachama wa Kisima cha Mafanikio Bi. Happyness Mushi amesema kuwa kabla hajajiunga na chama hicho alikuwa ni mshehereshaji asiyejua namna ya kupangilia shughuli zake,ila baada ya kujiunga amenufaika na Elimu ambayo inatolewa marakwamara amejifunza namna bora ya kuratibu matukio mbalimbali katika shughuli za kijamii,kiserikali kwa kuzingatia itifaki
Vilevile amesema kuwa anaiomba serikali kupitia barazaza la sana Mashirikisho mengine mbalimbali kuwatambua wafadhili matukio kwa kuwatupia jicho lapilli kama vile kwa wasanii mbalimbali wa filamu, vichekesho, wanamuziki.
Aidha Kisima cha mafanikio ni chama kilichosajiliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi mwaka 2020 chini ya sheria ya Jumuiya ya 337 kwa usajili Na.SA 21669 ili kujishughulisha na nyanja za kitaaluma, kijamii kiuchumi na kitamaduni,vilevile kinatambuliwa na Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo kupitia Baraza la Sanaa la Taifa kwa Sheria Na. 23 ya mwaka 1984 na kupewa kibali cha kuendesha shughuli za Sanaa Nchini Na.BST-9684-190.
Toa Maoni Yako:
0 comments: