Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akizungumza jambo wakati wa mafunzo kuhusu sheria za uchaguzi kwa Makamanda wa Polisi Wilaya (OCD) yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi (CCP). Kushoto ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji na kulia ni Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Selemani Mtibora.
Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika kuhakikisha inatoa Elimu ya Mpiga Kura kwa makundi mbalimbali katika jamii, leo Novemba 07, 2024 imetoa elimu hiyo kwa Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) nchini katika mafunzo yaliyofanyika katika Shule ya Polisi Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo ya siku moja kuhusu Sheria mbalimbali na Kanuni zinazoiongoza Tume, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani amesema kwa kuwapa elimu hiyo maafisa hao wa Polisi ngazi ya Wilaya kutasaidia kuondoa migongano baina yao na Vyama vya siasa.
“Kimsingi hawa ndio wasimamizi wa sheria ngazi ya Wilaya kutoka Jeshi la Polisi, hivyo tumewapitisha katika Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Sheria ya Rais, Wabunge na Madiwani ili iwawezeshe kuzitafsiri vyema hizi sheria na zitawawezesha katika usimamizi bora wa majukumu yao bila kuleta mtafaruku kati ya chama cha siasa au na wananchi kiujumla,” alisema Bw. Kailima.
Kailima amesema kwa sasa Polisi wanajua Wajibu wao ni nini na chama cha siasa kinatakiwa kufanya nini wakati huu ambapo Tume inaendelea na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini.
Aidha, Kailima amesema wakati wa kuelekea uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Tume itakutana tena na Jeshi hilo na kuwapa ufafanuzi juu ya mambo mbalimbali yahusuyo Uchaguzi Mkuu ili kuendelea kuwa na uchaguzi mkuu wa amani, huru na haki na kuwezesha baada ya uchaguzi Mkuu hali inaendelea kuwa ya utulivu.
Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji amesema lengo la mafunzo hayo ni kuliweka tayari Jeshi la Polisi wakati wa mchakato wa uchaguzi na kwa kuzingatia kuwa wao ndio wasimamizi wa sheria na walinzi wa raia na mali zao wakati wote.
CP Awadhi amesema Tume imewapa elimu juu ya wajibu wa Polisi katika shughuli za uchaguzi, sheria na kanuni mbalimbali wakati huu wa uboreshaji na lengo ni kujipanga na kuhakikisha mazoezi yanayoendelea nchini yanafanyika katika hali ya usalama mkubwa.
Mafunzo hayo ya siku nne ya Wakuu wa Polisi Wilaya Nchini yaliyoanza Novemba 4, 2024 yanataraji kufikia tamati Novemba 8 mwaka huu ambapo mada mbalimbali kuhusu uchaguzi na ushiriki wa jeshi la Polisi zimetolewa.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, CP Awadhi Juma Haji wakati wa mafunzo hayo
Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Selemani Mtibora akizungumza wakati akiwasilisha mada kuhusu Sheria mbalimbali za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi.h
Mkurugenzi wa Daftari na TEHAMA wa Tume, Bw. Stansalaus Mwita akiwasilisha mada ya mifumo wakati wa mafunzo hayo.
Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi ambao ni Wakuu wa Polisi Wilaya wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi ambao ni Wakuu wa Polisi Wilaya wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi ambao ni Wakuu wa Polisi Wilaya wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi ambao ni Wakuu wa Polisi Wilaya wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Majadiliano pia yalifanyika na Makamanda hao wa Polisi Wilaya (OCD) walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.
Majadiliano pia yalifanyika na Makamanda hao wa Polisi Wilaya (OCD) walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa maoni.
Toa Maoni Yako:
0 comments: