Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akizungumza wakati wa ziara yake katka Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Pwani ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na taarifa ya kina ya mradi wa Tanzani ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, Mikocheni jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Septemba, 2024.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akipokea taarifa kutoka kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi Peter Mwasalyanda kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na taarifa ya kina ya mradi wa Tanzani ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini wakati wa ziara yake katika ofisi hizo za Kanda ya Pwani zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Septemba, 2024.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akizungumza wakati wa ziara yake katka Ofisi za Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Kanda ya Pwani ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo pamoja na taarifa ya kina ya mradi wa Tanzani ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, Mikocheni jijini Dar es Salaam leo tarehe 10 Septemba, 2024.

Na Mwandishi Wetu.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb), amewataka viongozi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kutumia vyombo vya habari ili kutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na mfuko huo.

Mhandisi Mahundi amesema hayo tarehe 10 Septemba, 2024, wakati wa ziara yake katika ofisi za UCSAF Kanda ya Pwani zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam, ambapo alikagua shughuli mbalimbali pamoja na mradi wa Tanzania ya Kidijitali wa ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini.

 “Mahusiano na vyombo vyetu vya habari ni muhimu, Ukifanya kazi ukikaa nayo, hakuna atakayejua umefanya hivyo. Ni muhimu kuvishirikisha katika utekelezaji wa shughuli zenu mbalimbali,” amesisitiza Mhandisi Mahundi.

Aidha, Naibu Waziri huyo amehimiza UCSAF kuwashirikisha viongozi mbalimbali, wakiwemo wabunge, wanapotoa huduma za mawasiliano katika maeneo yao. 
Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia katika kupata taarifa sahihi za maendeleo katika maeneo husika.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Mahundi amesisitiza umuhimu wa kuongeza kasi katika ujenzi wa minara 758 ya mawasiliano vijijini, akieleza kuwa kumekuwa na mahitaji makubwa ya mawasiliano katika maeneo mengi.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF, Mhandisi Peter Mwasalyanda, amesema tayari wameshakaa kikao na kampuni za simu na kuweka utaratibu mzuri wa kukamilisha ujenzi wa minara hiyo, pamoja na kuongeza nguvu katika kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli zinazofanywa na mfuko huo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: