Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) unaofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo Jijini Arusha tarehe 11 hadi 12 Juni, 2024.
Mhandisi Mahundi atafungua mkutano huo tarehe 11 Juni, 2024 unaotarajiwa kujadili maazimio na taarifa za vikao vya Kamati za Wataalam wa masuala ya posta vilivyoanza tarahe 03 Juni, 2024 vilivyojadili masuala mbalimbali yanayohusu Fedha na Utawala, Mkakati, Sera na Kanuni, pamoja na Uendeshaji na Teknolojia.
Mkutano huu utahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Posta kutoka barani Afrika na wajumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Posta Duniani.
Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya Sekta ya Posta barani Afrika likiwa na jukumu la kuziunganisha nchi wanachama katika kupata fursa, kujadili changamoto na kutafuta suluhu endelevu kwa ajili ya kuboresha huduma za posta katika mataifa 45 wanachama.
Toa Maoni Yako:
0 comments: