Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Chritine Grau, aliyefika Ofisini kwa Waziri wa Fedha kwa ajili ya kujitambulisha, katika Ofisi Ndogo za Hazina jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana namna ya kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupitia misaada ya kibajeti na miradi mingine ya maendeleo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza wakati wa kikao chake na Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Chritine Grau, aliyefika Ofisini kwa Waziri wa Fedha kwa ajili ya kujitambulisha, katika Ofisi Ndogo za Hazina jijini Dar es Salaam, ambapo wamejadiliana namna ya kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupitia misaada ya kibajeti na miradi mingine ya maendeleo.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (watano kushoto) na Balozi Mpya wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Chritine Grau (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na Ubalozi wa Umoja wa Ulaya nchini baada ya kikao chao, katika Ofisi Ndogo za Hazina jijini Dar es Salaam, ambapo Balozi huyo alifika kujitambulisha na pia kujadiliana namna ya kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupitia misaada ya kibajeti na miradi mingine ya maendeleo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)

Na Benny Mwaipaja, Dar es Salaam

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa kutenga zaidi ya EURO milioni 703 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha miaka 7 kuanzia mwaka 2021 hadi mwaka 2027.

Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi mpya wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Mhe. Chistine Grau aliyefika kujitambulisha rasmi.

Mhe. Dkt. Nchemba alisema kuwa fedha hizo zimegawanywa katika awamu mbili ikiwemo awamu ya kwanza ya kipindi cha miaka 4 ilitengewa zaidi ya euro milioni 426 ambapo mpaka sasa Umoja huo umetoa zaidi ya euro milioni 373 ambazo zimeelekezwa katika miradi kadhaa ikiwemo uchumi wa buluu, ujenzi wa miji ya kisasa, upatikanaji wa mitaji, utawala wa fedha, upatikanaji wa mitaji kwa sekta binafsi, usawa wa kijinsia na mradi wa kuendeleza masuala ya kidigiti.

Aliiomba EU kuangalia uwezekano wa kutumia sehemu ya fedha, zaidi ya euro milioni 200 zitakazotumika katika awamu ya pili ya program hiyo itakayoanza mwakani kitumike kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya barabara ya kutoka Mikumi hadi Kidatu yenye urefu wa kilometa 35 ili kuchochea uchumi na maendeleo ya wakazi watakaonufaika na barabara hiyo.

Kwa upande wake, Balozi mpya wa Umoja wa Ulaya, Mhe. Christine Grau, alisifu mageuzi makubwa ya kiuchumi na kijamii yanayoendelea nchini kupitia kwa ungozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya MUungano wa Tanzania, yaliyoifanya Tanzania kuendelea kuwa imara na kuvutia uwekezaji na mitaji kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Aidha, Mhe. Balozi Grau aliarifu kuwa majadiliano ya awali ya ushirikiano mwingine wa miaka 7 unaotarajiwa kuanza mwaka 2028 hadi 2034 yataanza rasmi mwakani 2025.

Mhe. Balozi Grau aliipongeza Tanzania kwa kuridhia na kusaini mkataba mpya wa ushiriakiano kati yake na Umoja huo ujulikanao kama SAMOA ambao pamoja na mambo mengine utaiwezesha Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya kuendelea kufanyakazi zake nchini.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: