Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akishuhudia makabidhiano ya ofisi kati ya aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Everisto Longopa (kulia) ambaye kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, ya vitendea kazi Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya, Balozi Prof. Kennedy Gaston. Hafla hiyo fupi iliyofanyika katika Makao Makuu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mtumba jijini Dodoma Septemba 20, 2023.Hafla hiyo pia ilihusisha kumuaga Dkt Longopa.
Jaji Dkt. Longopa akizungumza wakati wa hafla hiyo na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Balozi Prof. Gaston.
Balozi Prof. Gaston akitoa neno la shukrani baada ya kukabidhiwa ofisi na Jaji Dkt. Longopa na kuomba ushirikiano na watumishi wa ofisi hiyo.
Mwandishi Mkuu wa Sheria wa ofisi hiyo, Onorius Njole akitoa neno la kumkaribisha Balozi Prof. Gaston kwa niaba ya watumishi wa ofisi hiyo na kuahidi kwamba watumishi wako tayari kutoa ushirikiano kwake.
Mkurugenzi wa Divisheni ya Uratibu na Huduma za Ushauri wa ofisi hiyo, Dkt. Gift Kweka akitoa neno la kumkaribisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mhe. Jaji Dkt. Feleshi kuzungumza wakati wa makabidhiano hayo.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi akizungumza wakati wa makabidhiano hayo na kuwataka watumishi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Balozi Prof. Gaston.
Mwanasheria Mkuu wa Seikali (AG), Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (katikati) akiwa na Balozi Prof. Gaston (kulia) pamoja na Jaji Dkt. Longopa.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA
0754264203
Toa Maoni Yako:
0 comments: