Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo na Kata kutoka Halmashauri sita za Tanzania Bara wapo katika mafunzo ya usimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Udiwani yanayofanyika jijini Tanga. Mafunzo hayo yanahudhuriwa na washiriki 44.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na Majukumu ya Watendaji wa uchaguzi na mambo muhimu ya kuzingatia, Uteuzi wa wagombea na fomu zinazotumika katika uteuzi, pingamizi na rufaa.

Mada nyingine ni Maadili na Kampeni za Uchaguzi, Wajibu na majukumu ya watendaji wa vituo na utambulisho wa mawakala wa vyama vya Siasa, Taratibu za upigaji kura, ufungaji wa vituturi na masanduku ya kura.

Aidha washiriki walipata fursa ya kufundishwa taratibu za kuhesabu kura kituoni, kujumlisha na kutangaza matokeo ya udiwani, Fomu zinazotumika wakati wa kupiga kura na kujumlisha kura.

Pia mada za mapokezi na utunzaji wa vifaa, mapokezi na matumizi ya fedha za uchaguzi ziliwasilishwa.

Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mdogo wa Kata 14 za Tanzania Bara unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 Julai, 2023 kujaza nafasi wazi za madiwani.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Kata zinazotarajiwa kufanya uchaguzi mdogo ni pamoja na Ngoywa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Kalola iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Sindeni iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Potwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Kwashemshi iliyopo Halamshauri ya Wilaya ya Korogwe, Bosha iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Mahege iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti na Bunamhala iliyopo katika Halmashauri ya Mji wa Bariadi.

Nyingine ni, Njoro na Kalemawe zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Same, Mnavira iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Kinyika iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Magubike iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa na Mbede iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Washiriki wakifanya mafunzo ya vitendo ya ufungaji vituturi vya kupigia kura.
Mkufunzi Mawazo Bikenye kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (kulia) akielekeza namna ya ufungaji wa sanduku la kura.
Washiriki wakifanya majaribio ya kufunga sanduku kwa kutumia rakili
Mshiriki akionesha namna ya Sanduku la Kura linavyopaswa kufungwa.


Mkurugenzi wa Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar, Adam Mkina akiwasilisha mada kuhusu kujumlisha na kutangaza matokeo ya Udiwani.

Afisa wa Tume, Michael Simba akiwasilisha mada ya taratibu za kuhesabu kura kituoni.
Afisa wa Tume,Mawazo Bikenye akiwasilisha mada kuhusu taratibu za upigaji Kura na mazoezi ya ufungaji vituturi na masanduku ya Kura.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Afisa wa Tume, Tumaini Ng'unga nae akitoa mada
Afisa wa Tume Amos Madaha akiwasilisha mada kuhusu fomu zinazotumika wakati wa kupiga Kura, Kuhesabu Kura na Kujumlisha Matokeo.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: