Wadau mbalimbali wa Mazingira wametakiwa kuyalinda na kuyatunza Mazingira kwa kupanda miti katikati katika maeneo mbimbali ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali za kutunza mazingira.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hashim Komba wakati akizungumza na waandishi wa Habari jana akizindua kampeni ya awamu ya kwanza ya ' Mti Wangu Tanzania Yangu' kwa lengo mahususi la kupanda miti 10, 000 kwa kipindi cha mwaka 2023/24 ambapo miti 5000 imepandwa katika eneo hilo.
"Mazingira tukiyatunza yatatuhifadhi na maisha yetu yatakuwepo na utunzaji wa mazingira unaanza na dhana ya upandaji wa miti, mabadiliko ya tabia ya nchi yanatokea kwasababu hatupandi miti na hatuitunzi miti hivyo tuwe na dhana ya kupanda miti ili kutunza mazingira"
Aidha alisema Rais Dkt. Samia amekuwa kinara wa Kutunza mazingira tangu alipokuwa Makamu wa Rais ambapo mwaka 2017 katika barabara ya Kilwa alizindua kampeni maamlum ya upandaji miti iitwayo ' Mti wangu' na kuhamasisha wananchi kupanda miti.
Kwa upande wake Dennis Katto kutoka Fanikiwa microfinance company LTD na Platnum Credit LTD alisema katika kuunga jitihada za serikali katika kutekeleza agizo kwa kila Halmashauri/ Wilaya la kupanda miti 1, 500, 000 kila mwaka kwa kushirikiana na Manispaa ya Ubungo Dar es Salaam katika kampeni iliyozinduliwa leo ya kupanda miti ya ' Mti wangu, Tanzaia Yangu' kwa lengo mahususi la kupanda miti 10,000 Kwa kipindi cha mwaka 2023/2024 kwa ushirikiano wa shirika lisilo la kiserikali la Human Dignity & Environment Care Foundation (HUDEFO).
"Tumeamua kuunganisha nguvu kuwa sehemu ya kukabili mabadiliko ya tabianchi kwa vitendo kwa kupanda miti na kuitunza ili kuchagia jitihada za kupunguza hewa ukaa duniani, kulinda na kupendezesha mazingira kwa ushirikiano wa serikali , jamii na wadau mbalimbali "
Kadhalika Katto alitoa wito kwa wadau wote kushiriki kwa pamoja katika kutatua changamoto za uharibifu wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi
Aidha Katto alitoa wito kwa sekta binafsi na sekta za kiraia kuitambua sekta ya mazingira kama kipimo cha maendeleo ya jamii na uchumi, kuendelea kuwekeza katika miundombinu yenye kulinda na kupendezesha mazingira nchini, lakini pia kuendelea kushirkiana kwa pamoja kukabiliana na mabdiliko ya tabianchi kwa kupanda miti na kuitunza, kutoa hamasa na uelewa wa jamii wa kulinda rasilimali ambazo ni kitovu cha ustawi wa uchumi wa nchi.
Naye mkurugenzi wa shirika la mazingira (HUDEFO) Sarah Pima alisema wao kama wadau wa mazingira serikali imekua ikishiriki kikamilifu katika kuhimili na kubaliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi hivyo tunapata nguvu zaidi kuendelea kushiriki kikamilifu katika uhifadhi na ulinzi wa mazingira.
Aliwaomba wadau wengine kushirikiana katika kuunga mkono juhudi za serikali na kuendelea kulinda afya zao.
Mweyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Ubungo Lobert Mbowe, alisema zoezi la upandaji miti lisiishie katika ofisi ya mkuu wa Wilaya pekee bali liendelee na sehemu mbalimbali ikiwemo mashuleni na hospitalini
Toa Maoni Yako:
0 comments: