Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
MBUNGE wa Jimbo la Mkinga (CCM) Dastan Kitandula ameishukuru Serikali kwa kuwapatia fedha bilioni 7 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na matumizi mengine kwenye Jimbo hilo .
Kitandula aliyasema hayo leo wakati akichangia Bajeti ya Kitandula-kuchangia bajeti ya Wizara ya Wizara ambapo alisema kwa upande wa barabara na miundombinu ya shule kwenye eneo walipangiwa kupata Bilioni 2 na wanapatiwa Bilioni 1.3 wanaomba fedha nyengine zilizobakia karibia milioni 700 zipatikane ili waweze kukamilisha miradi hiyo.
Alisema kwenye eneo la miundombinu ya shule wana milioni 692 wanakwenda kujenga shule mpya ya Msingi na Ujenzi wa Madarasa na matundu ya vyoo na wanazielekeza kwenye maeneo ya Maramba JKT,Mazola Kilifi,Mtimbwani,Kisiwani A na Perani hivyo wanaishukru sana Serikali
“Mh Spika kwenye eneo la Sekta ya Afya tunaishukuru Serikali kwa kutuanzishia ujenzi wa Hospitali ya wilaya tumeshaanza kutibu wagonjwa wa nje lakini bado changamoto ipo kwenye matibabu ya kibingwa kuwalaza wagonjwa na kufanya upasuaji ambao bado wanatumia hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo”Alisema
Mbunge huyo alisema kwamba wanaiomba Serikali iwapatie fedha wakamilishe ujenzi wa wodi na vifaa tiba katika Hospitali ya wilaya ya Mkinga ili wananchi waweze kupata huduma katika eneo hilo
Toa Maoni Yako:
0 comments: