Mgeni rasmi Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wametakiwa kuhakikisha wanatumia muda wa kazi kuiletea Taasisi yao manufaa badala ya kutumia muda huo kufanya mambo yasiyo na tija kwa muajiri.

Hayo yameelezwa leo Machi 11, 2023 na Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally wakati akifungua kikao kazi cha Chama cha Wafanyakazi wa Serikali kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

"Tunatambua umuhimu wa chama cha Wafanyakazi katika kuchagiza mafanikio ya mamlaka, rasilimali watu ni muhimu kwa maendeleo ya taasisi kwahiyo TUGHE ina wajibu wa kuhakikisha inazungumza vyema na watumishi wanaotoka nje ya mstari,"amesema Amina

Kiongozi huyo amewasisitiza Wafanyakazi kutumia muda wao wa kazi kwenye uzalishaji badala ya kutumia rasilimali za umma kwa maslahi yao, huku akikemea tabia ya baadhi ya watumishi wanaoangalia tamthilia na kukaa kwenye mitandao ya kijamii maofisini badala ya kufanya kazi.

Amesema vikao hivi ni muhimu kwa kuwa vinaleta mshikamano na umoja kwa wafanyakazi ikiwemo kujadili changamoto wanazozipata wafanyakazi na kuzitafutia ufumbuzi kwani wao ni kama daraja kati ya utawala na wafanyakazi.

Mbali na hayo, Amina aliwataka watumishi wa TCAA kuwasilisha changamoto wanazokumbana nazo kwa mamlaka husika badala ya kusubiri vikao vya TUGHE kueleza changamoto wanazopitia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la TCAA Jackline Ngoda, amesema lengo la kufanya kikao hicho ni kuwakumbusha watumishi wajibu wao katika utendaji ikiwa na kauli mbiu isemayo kuchaguza wafanyakazi wa usafiri wa Anga kufanya kazi kwa ufanisi na juhudi kwani hilo ndilo lengo la kuweza kuipaisha mamlaka hiyo.
Mwenyekiti wa TUGHE Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Jackline Ngoda akizungumza kuhusu namna wanavyoshirikiana na viongozi wa TCAA pamoja na kumkaribisha Mgeni rasmi Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally kwa ajili ya kufanya ufunguzi wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mwakilishi wa Katibu TUGHE mkoa Dar es Salaam Anthelmus Tarimo akitoa mada kuhusu umuhimu wa chama cha wafanyakazi mahali pa kazi pamoja na namna chama hicho kinachoweza kumlinda mfanyakazi hasa anapotaka kufukuzwa kazi au akiwa anefukuzwa kazi wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakichangia mada pamoja na kuuliza maswali kwa wawasilishwaji wa mada wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Mgeni rasmi Meneja Rasilimali Watu na Utawala Amina Silanda Ally akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: