Na Mwandishi Wetu
ZAIDI ya Sh.milioni 7.3 zinahitajika kwa ajili ya kumalizia Mradi wa ujenzi
ofisi ya Kata ya Kiparang'anda Mkoa was Pwani.
Akizungumza na wadau wa maendeleo katika kikao maalum cha maendeleo ,
Diwani wa kata hiyo, Shomari Mwambala ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti
Halmashauri ya Mkuranga, amesema, no wakati Sasa kwa wadau kujitokeza kuchagiza
maendeleo ili kata hiyo iiibuke kidedea
kwenye sekta mbalimbali.
Amesema lengo Hilo haliwezi kugikiwa endapo wadau watakaa pembeni na
kuwaachia viongozi peke yao hivyo no muhomu kujenga ushirikiano baina ya pande
zote hizo ambao utasaidia kuondoa
changamoto zilizopo.
Pia amesema tayari wapo kwenye mchakato wa kuboresha miundombinu ya
shule ndani ya kata hiyo ili kuongeza
ufaulu wa wanafunzi na hatmaye kufikia lengo la Serikali.
Ameongeza kuwa ili kufikia malengo hayo ni vema wadau wa maendeleo ndani ya
kata hiyo wakajitokeza kushiriki shughuli
za maendeleo lengo ikiwa ni pamoja na kujenga kata iwe bora ya mfano na
itasaidia kukuza ushirikiano was kimaendeleo.
"Wapo baadhi ya wadau wanafanya shughuli zao za maendeleo ndani ya
kata hii lakini baadhi yao wanajivuta kuchangia maendeleo hivyo ni muhimu
wakajitafakari vinginevyo hatua za kisheria zitaanza kuchukuliwa," amesema
Mwambala.
Mwambala amesema fedha nyingi za mikopo ndani ya halmashauri hiyo huwa
zinarejeshwa Serikali kuu kwa sababu waombaji wengi wanashindwa kutimiza
masharti.
Hata hivyo amewataka waombaji mikopo kutafakari aina nyingine ya miradi
kwakuwa waombaji wengi wamekuwa wakinunua bodaboda ambazo. zimekuwa
zikisababisha athari ndani ya familia nyingi kuachwa yatima au ulemavu wa
kudumu.
Akizungumzia kuhusu awamu ya pili ya unganishwaji umeme ndani ya kata hiyo amesema unatarajiwa kuanza hivi karibuni ambapo tayari wataalam wamekwishafanya ukaguzi wa maeneo yatakayopitishwa umeme.
Awali bajeti za halmashauri iliyopita ilikuwa ni kuendeleza kata zake
ambapo fedha hizo hazikutosheleza kumaliza miundombinu ya ofisi hiyo.
" Bajeti ya mwaka huu haina ofisi ya maboresho ya kata...iliyopo
imelenga zaidi kwa kata ambazo hazina majengo," amesema Mwambala.
Naye, Ofisa Mtendaji wa kata hiyo, Zawadi Jadi amesema ufinyu wa mapato ndani ya kata hiyo umechangia kushindwa kumaliza kwa wakati ofisi ya kata hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments: