MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga ambao hawapo pichani kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga kuhusu kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuimarisha Demokrasia nchini
Na Oscar Assenga,TANGA
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake UWT Taifa Mary Chatanda amesema UWT imekoshwa na uamuzi wa kihistoria wa Rais Dkt Samia Suluhu kuondoa zuio la mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa nchini maamuzi ambayo yameleta faraja kwa vyama hivyo na hivyo kufungua ukurasa mpya wa demokrasia nchini
Chatanda aliyasema hayo leo kwenye ofisi za CCM Mkoa wa Tanga wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali kuhusu kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa nchini ambapo
Alisema kwamba UWT imekoshwa na hatua ya kihistoria kuondoa zuio la mkutano ya hadhara vyama vya siasa ikiwemo kukwamua mchakato wa kupata Katiba mpya ambapo alisema kwamba wao wanaunga mkono uamuzi wa Kukwamua mchakato wa marekebisho ya Katiba ya Tanzania na hivyo tunahimiza amani na utulivu wakati wote wa kusubiri Serikali kukamilisha taratibu zote za kuanza mchakato huu kama alivyoeleza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan katika hotuba yake jana tarehe 3 Januari 2023.
Alisema pamoja na kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kupanua wigo wa demokrasia nchini ambapo alisema maamuzi ya Rais Dkt Samia yameleta faraja kwa vyama mbalimbali vya siasa nchini na kuwezesha kufikia hatu kubwa ya kidemokrasia nchini.
Aidha alisema Rais Dkt Samia ameendelea kuonyesha udhabiti wa kauli zake kwa matendo ambapo hata alipohutubia Taifa mara baada ya kuapishwa Maci 19,2022 alisema wakati huo sio wa kutazama mbele kwa mashaka bali ni kwa kutazama kwa matumaini mwisho wa kumnukuu.
Mwenyekiti Chatanda alisema maamuzi aliyoyafikia Rais Dkt Samia kupitia mchakato wa maridhiano kuanzia kuundwa Kikosi cha kazi pia mazungumzo kati ya Vyama vya Siasa na Vyama vya CCM na Chadema yameleta matumaini mapya katika kujenga demokrasia ya kuaminiana baina ya vyama vyote vya siasa nchini ambayo ni chachu katika ujenzi wa Taifa lenye umoja Amani a Utulivu.
“Lakini niwaambie kwanza falsafaya Rais Samia Suluhu ni kujenga upya nchi yenye umoja katika ujenzi wa Taifa inayoongozwa falsafa ya 4R maridhiano ustahimilivu,mabadiliko na kujenga upya nchi hadi sasa falsafa hiyo imefanikiwa kwa asilimia 100” Alisema Chatanda
Hata hivyo alisema sio tu kwa kuleta mafanikio makubwa ya kisekta aliyotekeleza Rais kwa muda mfupi wa chini ya miaka miwili madarakani licha kuipokea nchini ikiwa na hali tete ya kutokana majanga ya Corona ,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake mwaka 2021
“Kwa kweli sisi UWT tunasema Rais Dkt Samia amefanya jambo kubwa sana hivyo tunampongeza na hizo zinazotokana na matokeo ya mkutano baina ya Rais Samia na vyama vya siasa kwenye usajili wa kudumisha nchini,uwt wanampjgeza Rais Samia kwa kufanya maamuzi yalitileta furaha isiyo na kifani kwa wananchi wa Tanzania na wapenda Amani dunia kote kwa kutoa majawabu ya vikwazo vya demokrasia nchini wao na majanga ya korona,vita ya Ukraine na kufiwa na mtangulizi wake Mwaka 2021" Alisema Chatanda
Aliongeza kwamba bali falsafsa hìzo zinahimiza siasa za kustaarabu zenye kuweka watu pamoja,kujenga hoja za ushawishi kupitia majadiliano mazungumzo kuhusisha vyama vya siasa katika kuendesha nchi hivyo kutokana na hilo UWT wanampongeza Rais huku wakieleza kwamba hakika wanawake wanaweza.
Hata hivyo alisema kwamba Jumuiya hiyo ya UWT inawahimiza viongozi wanawake wa vyama mbalimbali kuandaa mikutano mingi ya hadhara ili kuweza kupokea changamoto mbalimbali zinazowagusa wanawake wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto zinazofanana bila kujali itikadi zao na pia katika mikutano wanapendeleza hatua mahususi za kuchukua kwa Serikali ili kumkomboa mwanamke kiuchumi,kijamii na kisiasa.
Mwenyekiti Chatanda alisema kwamba pia wamefurahishwa na uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita ya kuridhia mapendekezo ya kikosi kazi cha kufanya marekebisho ya sheria kadhaa ndani ya nchi kwa nia ya kuimarisha demokrasia zaidi ambayo yatahusisha wananchi.
Alisema wanaamini marekebisho hayo pia yatazingatia masuala ya usawa wa kijinsia katika kuongeza uwakilishi wa wanawake kwenye siasa na uongozi kuanzia kwenye vyama vya siasa kama ambayo wameshuhudia namna Rais Samia Suluhu alivyojitahidi kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye uongozi ndani ya Serikali yake na chama cha Mapinduzi
Mwenyekiti Chatanda aliwahimiza viongozi wake wa Jumuiya ya UWT kuanzia ngazi za Tawi ,Kata/Wadi ,Jimbo, wilaya , Mkoa mpaka Taifa pamoja na Madiwani,wawakilishi na Wabunge Wanawake kufanya mikutano ya hadhara kwa kufuata taratibu zote ,mikutano hiyo ilenge kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 , kusikiliza kero za wananchi na kujibu hoja mbalimbali zitakazopotoshwa kwa lugha ya kistaarabu na kwa kutumia takwimu sahihi , sisi Viongozi wa UWT Taifa tutaonyesha mfano kwa kutumia fursa hii iliyotolewa na Mhe Dk Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Hata hivyo pia alitumia nafasi hiyo kuitaka Jumuiya ya UWT kuendelea kuwaomba Watanzania kuendelea kumuamini Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na kumuunga mkono kwani ana dhamira njema ya kujenga Taifa linaloongea lugha moja , na ambalo kila mmoja anashiriki katika ujenzi wa Taifa lake .
Toa Maoni Yako:
0 comments: