Young Africans SC wamefuzu makumbi ya Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kupata ushindi jumla ya bao 1-0 dhidi ya Club Africain ya Tunisia, mchezo wa mkondo wa kwanza timu hizo zilitoka sare ya 0-0 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo bao la Young Africans lilifungwa na Mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kwenye dakika ya 78 ya mchezo wa mkondo wa pili uliopigwa kwenye dimba la Hammedi Agrebi Olympique - Rades mjini Tunis.

Young Africain imefuzu hatua ya makundi katika Michuano hiyo kwa mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2018, sasa hivi imefanya hivyo katika ardhi ya ugenini dhidi ya Club Africain.

Yanga SC wanaungana na Simba SC ambao wao wamefuzu hatua ya makundi ya Michuno ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuzitoa timu za Big Bullets ya Malawi na Club De Agosti ya Angola.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: