Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendanji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela tuzo ya Mkurugenzi Mtendaji (CEO/MD) Bora wa Mwaka 2022 Tanzania katika tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam. Wengine katika picha ni kutoka Tanzania Instute of Managers ambao ni Mwanzilishi mwenza (Co – founder) Deo John (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji, Alex Shayo (Kulia).
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Benki hiyo, Jesca Njau wakiwa na tuzo zao walizoshinda katika usiku wa tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), Afisa Mkuu wa Fedha wa Benki ya CRDB, Frederick Nshekanabo (wanne kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi wa Benki hiyo, Jesca Njau (wanne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja maafisa wengine wa benki hiyo wakati usiku wa tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es salaam.
Furaha baada ya ushindi.
Wadau
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Omar Shaaban (anayepiga makofi katikati), katika picha ni kutoka Tanzania Instute of Managers ambao ni Mwanzilishi mwenza (Co – founder) Deo John (anayepiga makofi kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (mwenye tuz nyekundu) wakiwa na washindi wa jumla na tuzo zao walizoshinda katika usiku wa tuzo za Top 100 Executive zilizofanyika tarehe 27 Novemba 2022 katika ukumbi wa Mlimani City, Jijini Dar es Salaam.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: