Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mheshimiwa Godwin Gondwe ameipongeza kampuni ya Simu ya Vodacom kwa kuwa mstari wa mbele kwenye kuleta mabadiliko yanayoigusa jamii moja kwa moja.

Akizungumza hapo jana Agosti 29,2022 alipotembelewa na washindi wa bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya ‘M Pesa imeitika’, Mheshimiwa Gondwe alitanabaisha kwamba Vodacom wamekuwa vinara katika mapinduzi ya teknolojia na huduma zinazonufaisha Watanzania wote.

“Vodacom walikua wa kwanza kufanya M PESA; Vodacom ilikua ya kwanza kuleta M-PAWA, Vodacom imeweza kuwa ya kwanza kuleta M-MAMA ambayo inasaidia kina mama kuweza kufika hospitalini haraka na wakapata huduma. Ni jambo kubwa sana. Lakini pia Vodacom walikua wa kwanza kuleta 4G. Kwa hiyo sisi kama Serikali tunawapongeza sana” amesena Mheshimiwa Gondwe.

Nao washindi wa zawadi za bajaji na pikipiki kupitia kampeni ya M-Pesa Imeitika, Magdalena Magoma na Beata Madachi, wameishukuru Serikali kwa kuweka mazingira wezeshi yanayoziwezesha sekta binafsi na kampuni kama Vodacom kuweza kuchangia maendeleo ya vijana kama wao na jamii kwa ujumla.

Aidha, Mheshimiwa Godwin Gondwe alisema kupitia ‘M Pesa Imeitika’ na huduma nyingine za Vodacom, vijana wanafikiwa na kuweza kutengeneza ajira akitolea mfano kwamba bajaji na pikipiki zilizotolewa zitatoa ajira kwa vijana.

Kampuni ya Vodacom inaendelea kuwa kinara kwa kuwa ya kwanza katika mapinduzi ya kidigitali na kuwa na huduma zenye ubora na kugusa maisha ya Watanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: