Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
WANACHAMA wa Timu ya Simba tawi la "Simba Tishio" Wilayani Kibaha Mkoani Pwani wametoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kwenye kituo cha Afya cha Mwendapole.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutoa misaada hiyo mwenyekiti wa tawi la Simba Tishio Ally Mkande alisema kuwa utoaji wa misaada hiyo ni sehemu ya wiki ya Simba.
Mkande alisema kuwa wameamua kujitolea kuwasaidia wagonjwa ambao wanapata huduma katika kituo hicho cha afya ili kuisaidia jamii.
"Tunaungana na timu yetu katika sherehe kwa kuwapatia wagonjwa sabuni na soda ili kuwafariji na kurudisha fadhila kwa jamii,"alisema Mkande.
Alisema kuwa wameamua kutoa misaada ili kungana na jamii bapo wao ni sehemu ya jamii na kuwataka watu wengine nao kujitolea.
"Timu nyingine nazo zifanye kama sisi ili kuisaidia jamii kwani nasi ni wanajamii na inaleta faraja kwa wale tunaowasaidia,"alisema Mkande.
Naye Zaina Mchabwa alisema kuwa amejisikia furaha kutoa msaada kwa wagonjwa kupitia tawi lao kwani wao ni mfano na wengine wafuate nyayo za timu yao.
Mchabwa alisema kuwa ni utamaduni wao kila mwaka kujitolea kwa jamii kwenye mambo mbalimbali kwa lengo la kushirikiana kwa kila hali.
Kwa upande wake mganga mfawidhi wa kituo hicho Daniel Laiser alisema kuwa ameguswa na tawi hilo kujitolea misaada kwa wagonjwa.
Laiser alisema kuwa timu mbali ya kutoa burudani pia zinapaswa kuisaidia jamii kwa kujitolea vitu mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments: