Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Maji Cup yanayofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kombezi Jijini Tanga kushoto ni Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shilloo kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shiloo akizungumza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayosimamia usambazaji maji (ATAWAS) Constantine Chiwalo akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo ya Maji Cup
Na Oscar Assenga,TANGA.
MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) katika mwaka wa fedha 2022/2023 wametenga milioni 990 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha wanapambana na upotevu wa maji.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Rashid Shabani wakati wa ufunguzi wa Mashindano ya Maji Cup yanayofanyika kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Kombezi Jijini Tanga.
Alisema fedha hiyo imetengwa kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali zikazopelekea kupunguza upotevu wa maji ambapo mwaka jana ulikuwa wastani wa asilimi 30 kwa kutekeleza hayo hiyo miradi wanaimani watapunguza upotevu huo hadi kufikia asilimia 26 June 2023.
Alisema kazi ambazo wanazilenga kuzifanya ni kuboresha miundombinu kwa ajili ya kuzibiti na kupunguza upotevu wa maji kutoka kwenye mabomba na watanunua na kufunga mita za malipo kabla hizo mita ni za aina yake na hivyo itakuwa mamlaka ya maji ya kwanza kuonyesha aina hiyo ya mita.
“Mita hizi tunatarajia tutaanza kuzifunga mwezi huu uzuri mita hizi kama kuna uvujaji mbele ya mita mteja anapata ujumbe kuna matumizi yanafanyika hebu fuatilia agizo hilo ni la wizara na sisi tunatekeleza kwa sababu tunataka kufunga mita ambazo ni rafiki kwa mtumiaji hiyo ni aina rafiki kwa sababu ina mjali mteja”Alisema
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema wamekuwa wakipokea malalamiko bili kubwa na moja ya chanzo ni maji kuvunja mbele ya mita hivyo hilo litakwenda kutatua hilo tatizo ikiwemo kuendelea kuelimisha jamii juu ya udhibiti wa upotevu wa maji na utoaji wa taarifa kwa mamlaka.
“Tunamshukuru Rais kutoa fedha zilizowezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayolenga kuondoa kero ya maji nchini na nyengine nga imeshaleta mabadiliko makubwa ya utapatikanaji wa huduma ya maji nchini ikiwemo Jiji la Tanga ambapo kwa sasa imefikia asiimia 97”Alisema
Hata hivyo alisema Serikali itoa bilioni 13.31kwa ajili ya kujenga miradi ya maji kuhakikisha wananchi wa Jiji la Tanga wanapata huduma ya maji safi na salama.
Alisema pia wamepenga kutanua mtambo wa kusafisha maji eneo la Mowe ambapo wametenga Bilioni 9.1 na kwa sasa unaendelea na umefikia asilimia 62.
“Lakini pia tumeendeleza mtandao wa mabomba kilimota 17.6 maeneo ya Kichangani,Pongwe,Masiwani na Neema huu ni mradi wa kukabiliana na ugonjwa wa Uviko na umekamilika asilimia 100 ulikuwa na thamani milioni 500”Alisema
Kaimu Mkurugenzi huyo alisema licha ya hivyo serikali imewezesha fedha kujenga mradi wa maji kufikisha huduma maeneo ya Kibafuta,Mleni ,ndaoya,mpirani na chongoleani na kata ya chongoleani ni eneo pekee la Jiji la Tanga ambalo lilikuwa halina mtandao wa huduma ya maji sasa miundombinu imefika na wananchi na wameanza kupata huduma hiyo ya maji.
“Mradi hu wa kupelekea maji Chongoleani una thamani ya Milioni 918 na utekelezaji mradi umefikia asilimi 90 lakini pia kuna mradi wa kulaza bomba kubwa kuboresha hali ya upatikanaji wa maji katika eneo hilo ”alisema
Alieleza hiyo inatokana na wananchi wa eneo la Chongoleani kupata maji kwa mgawo na serikali imetoa bilioni 2.7 kwa ajili ya kulaza bomba kubwa kutoka eneo la Amboni mpaka Chongoleani ili kuhakikisha wanapata maji muda wote.
Toa Maoni Yako:
0 comments: