Kampuni inayoongoza kimataifa katika kubashiri michezo mtandaoni, Betway ambayo ni sehemu ya Super Group, imekarabati na kuzindua kiwanja kingine cha mpira wa kikapu kilichopo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo umefanyika Jumamosi, tarehe 26 Machi 2022 ikiwa ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo kuboresha ya vituo vya michezo unaolenga kukarabati viwanja 5 vya mpira wa kikapu jijini Dar es Salaam.
Kupitia mradi huo, Betway inakarabati viwanja vya mpira wa kikapu katika vituo vya michezo vya umma kwa nia ya kuongeza thamani ya mchezo wa mpira wa kikapu nchini.
Ili kuhakikisha viwanja vilivyokarabatiwa vinatunzwa ipasavyo kwa matumizi endelevu, Betway inashirikiana na Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF)–chombo cha serikali chenye jukumu la usimamizi wa mpira wa kikapu nchini.
TBF ina jukumu kubwa katika kuhakikisha kuwa viwanja hivi vinatumika ipasavyo kwa mashindano ya mpira wa vikapu na shughuli zingine zinazohusiana na mchezo huo.
Hafla hiyo ya uzinduzi imeenda sambamba na bonanza lililowaleta pamoja zaidi ya watu 250 na wadau kutoka sekta ya mchezo wa mpira wa kikapu wakijumuika kushuhudia uzinduzi wa kiwanja hicho.
Tukio kuu la bonanza hilo lilikuwa ni mchezo wa mpira wa kikapu kati ya timu 2 za kike, Dar Queens na Dar Divas wakiwania kitita cha THS 500,000. Betway iliwapa kipaumbele wanawake kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka.
Akizungumza na washiriki wa hafla ya uzinduzi, Afisa Masoko wa Betway Tanzania, Calvin Mhina, alieleza kwa ufupi lengo la Betway kufanya maboresho ya viwanja.
"Tulichukua jukumu la kuongeza hadhi ya uwanja huu (Leaders Club) kwa kuzingatia thamani itakayoongeza kwenye mchezo wa mpira wa kikapu kwani huu ni moja ya viwanja maarufu vya michezo na burudani jijini Dar es Salaam. Betway tunaamini kuwa maendeleo ya jamii ni sehemu ya majukumu yetu ya msingi na tutaendelea kusaidia jamii ya wanamichezo katika nyanja zote za maendeleo ya michezo,” alisema Mhina.
Katibu Mkuu wa TBF, Mwenze Kabinda, alipongeza hatua ya Betway huku akikiri kuwa kuboreshwa kwa viwanja hivyo kutaongeza thamani kubwa ya mchezo huo.
Katibu Mkuu wa TBF, Mwenze Kabinda alipongeza hatua ya Betway huku akikiri kuwa kuboreshwa kwa uwanja huo kutaongeza thamani kubwa ya mchezo wa mpira wa kikapu.
“Tukiwa kama shirikisho linalohusika na maendeleo ya mchezo huu, ni furaha kubwa kwetu kuona wadau kama Betway wanawekeza katika kuboresha miundombinu ambayo ni muhimu katika kuhakikisha maendeleo ya mchezo wowote ule. Tunashukuru kwa mradi huu na hii inaleta msukumo kwetu kama mamlaka husika kuja na mashindano zaidi ili kuhakikisha viwanja hivi vinatumika", alisema Mwenze.
Wachezaji wa mpira wa kikapu, wapenzi na wadau walioshiriki katika bonanza hilo walifurahi sana kutazama mchezo huo na kushiriki katika matukio mengine ya kuburudisha. Wachezaji pia walielezea furaha yao juu marekebisho ya uwanja waliyoyaona na kuwa sehemu ya uzinduzi kwa kucheza.
Toa Maoni Yako:
0 comments: