Na Said Mwishehe, Michuzi TV

BAADA ya kuonekana idadi ya watu wanaotaka kusajili majina ya biashara,majina ya Kampuni pamoja na kurasimisha biashara zao, Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umetangaza kuongeza muda wa utoaji Elimu na Huduma katika eneo la Mlimani City Jijini Dar es Salaam hadi siku ya jumatano Februari 2, 2022

BRELA walianza kutoa huduma ya kutoa elimu na kuhudumia wananchi Januari 26 mwaka huu na walipanga kumaliza Januari 30 lakini kutokana na watu wengi kuhitaji kuhudumiwa Wakala huo wameamua kuongeza muda wa kutoa huduma hadi Jumatano ya Februari 2,2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Kitengo Cha Uhusiano na Mawasiliano cha BRELA kimesema baada ya kuona mahitaji ni makubwa wameamua kuongeza muda wa kuhudumia wananchi kupitia Wiki ya utoaji elimu kwa umma.

Kitengo hicho kimefafanua awali kilitenga siku tano za kutoa huduma katika Viwanja vya Mliman City lakini tangu waanze kuwahudumia wananchi wamekuwa wakijitokeza kwa Hivyo imeongeza siku tatu ili kuendelea kutoa huduma kwa ufanisi zaidi.

Taarifa hiyo imefafanua kwamba "hatua hiyo ya kuongeza siku imetokana na wadau wengi kujitokeza kwa wingi kupata huduma zinazotolewa na BRELA katika muda wa siku tano zilizopangwa awali hivyo kulazimu kuongeza muda wa siku tatu ili kuendelea kutoa Huduma kwa ufanisi zaidi".

BRELA katika kampeni hiyo wamejikita katika kutoa kuhusu umuhimu wa wafanyabiashara kurasimisha biashara zao,kusajili Kampuni pamoja na majina ya biashara na kubwa zaidi wamekuwa wakitoa maelekezo na kutatua changamoto zinazowakabili katika ujazaji nyaraka za Wakala huo.

Hata hivyo BRELA wamewaomba wananchi wanaohitaji kuhudumiwa na Wakala huo kwenye mambo mbalimbali kufika viwanja vya Mliman City ili wahudumiwe na maofisa wa Wakala huo wamejipanga katika kuhakikisha wote wanaofika wanapata huduma.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: