Mchezaji chipukizi Isack Daudi kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo akikabidhiwa kombe na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Ally Possi baada ya kuibuka mshindi wa jumla mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku wa Disemba 5, 2021 akitoa hotuba ya kufunga rasmi mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku wa Disemba 5,2021 akikabidhiwa kanuni za mchezo wa Gofu na Mwenyekiti wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Brigadia Generali Mstaafu, Michael Luwongo baada ya kutangaza nia ya kujifunza mchezo huo.

Na. John Mapepele

Naibu Katibu Mkuu wa WizarayaUtamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt, Ally Possi usiku waDisemba 5, 2021 amefunga rasmi mashindano ya Golfu ya NBC Tanzania Open 2021 jijini Dar es Salaam na kukabidhiwa kanuni za mchezo huo na Mwenyekiti wa Klabu ya Jeshi ya Lugalo Brigedia Generali Mstaafu, Michael Luwongo baada ya kutangaza nia ya kujifunza mchezo huo.

Katika mashindano hayo mchezaji chipukizi Isack Daudi kutoka Klabu ya Gofu ya Lugalo ameibuka kuwa mshindi wa jumla wa mashindano ya mwaka 2021. 

Akifunga mashindano hayo, Dkt. Possi amepongeza vilabu kwa kuanza kuwekeza na kuibua vipaji kwa watoto ambao wameshiriki mashindano ya mwaka huu kwa mara ya kwanza na kufanya vizuri.

Akimkaribisha kufunga mashindano hayo, Mwenyekiti wa Chama cha Gofu Tanzania (TGU), Chriss Martin ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kudhamini wa Timu ya Taifa ya mchezo wa Gofu ili iweze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa na pia ameomba kiwanja kwa ajili ya mchezo huo. 

Akijibu maombi hayo, Dkt. Possi amefafanua kuwa Serikali ina mikakati kabambe ya kuendeleza michezo ikiwa ni pamoja na kutoa udhamini kwa timu za taifa za michezo zinazofanya vizuri kupitia Mfuko wa Michezo ulioanzishwa hivi karibuni endapo zitakuwa zimekidhi  vigezo vilivyowekwa.

Ameongeza kuwa Serikali pia itazingatia kigezo cha utawala bora kwenye vyama na mashirikisho ya michezo katika kudhamini michezo huku akitoa wito kwa vyama kuwa na utawala bora ili kufika katika ngazi ya kimataifa.

Akizungumzia kuhusu kiwanja amesema  Serikali ipo tayari kuwatafutia  kiwanja kwa ajili ya Gofu ambapo amesisitiza kuwasilisha  maombi rasmi yafanyiwe kazi ili wapatiwe  kiwanja  hicho.

Akitoa Salamu za Waziri waUtamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Innocent Bashungwa amesema amemuagiza TGU kukutana mara moja na Mhe. Waziri Bashungwa ili kujadilia na namna ya kuuendeleza mchezo huo pendwa ambao umeonyesha kukuwa kwa haraka hapa nchini.

Katibu wa mashindano hayo, Mhandisi Enock Magile amesema TGU katika kuendeleza mchezo huo kimeandaa michezo maalum ya Gofu kwa akina mama itakayofanyika mwakani. 

Aidha amesema Aprili 2022, Tanzania itakuwa mwenyeji washindano la kimataifa la mchezowaGofu la Europen Tour Challenge litakalowaleta wachezaji wa kimataifa 159 kutoka mataifa mbalimbali duniani watakaoambatana na wageni 559 ambapo amefafanua kuwa litasaidia  kukuza  utalii.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: