Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

Waziri wa Nishati Mhe. January Y. Makamba (Mb), amewasilisha Ujumbe Maalum wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenda kwa Mhe. Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Waziri Makamba amewasilisha ujumbe huo maalum kupitia kwa Mhe. Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, tarehe 24 Oktoba, 2021 katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya UAE.

Makamba yupo Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ziara ya kikazi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika masuala ya Mafuta na Gesi.

Mhe.Makamba katika mazungumzo hayo ameambatana na Mhe. Mohamed Mtonga, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu, Kamishina wa Mafuta na Gesi, Ndg. Michale Mjinja kutoka Wizara ya Nishati pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: